Hospitali ya wilaya ya Kiteto inajenga majengo matatu ya thamani ya sh 900 mil zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, fedha ambazo zimelenga kuboresha hospitali chakavu hapa nchini ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 35%.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kiteto, John Nchimbi Leo Aprili 12.2023 ametaja majengo hayo kuwa ni jengo la upasuaji, jengo la mama na mtoto, chumba na maabara.
"Rais Dr. Samia Suluhu Hassan ameamua kuboresha hospitali za wilaya kongwe hapa nchini, ikiwemo hospitali yetu ya Kiteto ambapo sisi tumeamua kujenga majengo muhimu matatu ya thamani ya 900 mil, jengo la maabara, mama na mtoto na upasuaji"
"Mhe Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo katika ziara yake ya hivi karibuni Kiteto aliipongeza halmashauri kwa wazo lao la kujenga majengo matatu hospitali ya Kiteto badala ya kupaka paka rangi majengo ya miaka 70 ambayo hayafai tena kwa wakati huu"
"Sh 900 mil tulizopewa halmashauri ya Kiteto tunajenga jengo la mama na mtoto, tunajenga chumba cha upasuaji kilichokuwepo awali ni cha miaka ya 70 kwa kweli hakifai na hakikuwa kwa ajili ya kazi hiyo kilikuwa kwa ajili ya kukidhi mazingira ya wakati huo na jengo la maabara ambalo wilaya haikuwa nalo" alisema
"Kwa sasa haya majengo matatu yatawezesha hospitali ya Wilaya ya kiteto iendane na kasi ya sasa, kati ya hospitali zinazofanana na kipindi hiki cha mama Samia Suluhu Hassan ambazo ni bora kabisa hapa nchini"alisema Nchimbi
Amesema kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 35% akiamini kuwa fedha hizo zitakamilisha majengo hayo yote matatu tofauti na wilaya zingine ambazo wao walipewa sh 1.1 bil
"Kiteto tumejipanga kumaliza ujenzi kwa kununua vitu kutoka viwandani kwa bei nafuu na kuhakikisha kuwa majengo hayo yanakuwa na ubora ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo ya Afya" alisisitiza Nchimbi
Amesema baada ya majengo hayo matatu kukamilika hospitali hiyi itakuwa inahitaji majengo mengine matano na kufanya hospitali kuwa na majengo mapya na kisasa kama hospitali zingine kipindi hiki cha awamu ya sita ambacho kinakazania kujenga hospitali bora hapa nchini
Mwenyekiti wa bodi ya Afya ya Afya Kiteto Ibrahimu Mussa alimshukuru Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa sh 900 mil za kukarabati hospitali ya Kiteto iliyojengwa miaka 70 iliyopita kwa kujenga majengo matatu muhimu ambayo wakati mwingine inalazimu wagonjwa kupelekwa hospitali za nje ya wilaya.
Erika Ndorosi (mwananchi) Kijiji cha Kaloleni amezungumzia huduma inayotolewa katika hospitali hiyo na kupongeza Rais Dr Samia Suluhu Hassan kutoa fedha hizo na kuanza kujenzi akisema kuboreshwa huduma hizo kutapunguza vifo vya mama na mtoto.
Post A Comment: