Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) katika Msitu wa Mafunzo Olmotonyi- Arusha kimeendelea na utunzaji mzuri wa mazingira lengo likiwa ni kuhuisha mazao yatokanayo na misitu.
Kaimu meneja wa Msitu wa Mafunzo Olmotonyi Bw. Saidi Kiparu amesema Msitu ulikabidhiwa kimeanzishwa mwaka 1978 kwa ajili ya mafunzo, utafiti, ugani na uzalishaji mapato. Kituo kina ukubwa wa hekta 865 ikiwa na Hifadhi ya Msitu wenye hekta 840 na hekta 25 za makazi. Msitu una spishi 11 za miti yakupandwa na hifadhi miti ya uoto wa asli.
Aidha ameeleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chuo ni kutoa mafunzo kwa vitendo kwa ngazi za Shahada za Misitu ,Uandaaji wa shamba la miti, utunzaji na ulinzi wa msitu kwa ushirikiano na wananchi waishio karibu na msitu ambao hulima mazao ya muda mfupi kwenye msitu kwa ajili ya kijipatia chakula.
Mara baada ya miti kuwa na umri wa miaka 18 miti husika huanza kuvunwa magogo na kuyachakata kwenye mashine tatu laimet, Kara, na Slidetec ambazo zina uwezo wa kuzalisha mbao mita za ujazo 30 kwa siku.
Slidetec ni mashine mpya ya kisasaSawmill iliyonunuliwa mwaka 2023 na ina uwiano mkubwa wa kuchakata magogo kupata mbao safi asilimia 48-50 wakati mashine nyingine huchakata mbao kwa asilimia 33-40 hali ambayo ni mafanikio kwao katika uboreshaji Teknolojia mpya na kurahisha majukumu ikiwemo na kupunguza gharama za matengenezo na uendeshaji..
Matarajio makubwa kwa Chuo katika kituo cha Mafunzo Olmotonyi ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya Misitu ili kupata fedha kusaidia kuendesha kituo na kuchangia mapato serikalini kutokana na mauzo ya mazao ya misitu huo wa mafunzo
Vilevile Menejimenti ya Chuo imendelea kuboresha miundo mbinu mbalimbali ya kituo ili kiendelee kuwa bora zaidi kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi na kutoa wataalamu bora wa masuala ya misitu na fani zingine
Kwa mujibu wa makamo wa Rais Mhe. Philip Isdory Mpango amekua akihamasisha utunzaji wa mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoweza kuleta athari kwa jamii.
Post A Comment: