Julieth Ngarabali. Pwani
Zaidi ya sh.470 milioni zimetengwa kwaajili ya shule mbalimbali za sekondari nchini zitakazofanikiwa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan ya utunzaji mazingira na matumizi sahihi ya Nishati mbadala kwa kupanda miti na kuitunza kwa asilimia 80.
Akizungumza Wilayani Kibaha kwenye uzinduzi wa kampeni ya utunzaji mazingira na matumizi ya nishati mbadala Kaimu Meneja wa benki ya NMB kanda ya Dar esalaam, Seka Urio amesema fedha hizo zimetegwa na NMB kwa lengo la kuongeza chachu ya upandaji miti na utunzaji mazingira hatua itakayochangia kurejesha uoto wa asili na kupambana na uharibifu wa mazingira unaobabishwa na vitendo vya ukataji miti hivyo.
Urio amesema fedha hizo zitatolewa kama zawadi kwa viwango tofauti kwa mshindi wa kwanza mpaka watatu pamoja na shule zote zitakazoshiriki kampeni hiyo nazo zitashikwa mkono ambapo zitapata sh.2 milioni pamoja na cheti cha ushiriki.
"Shule itakayopanda miti 2,000 na kuitunza ikakua kwa asilimia 80 itaingia kwenye shindano na mshindi atazawadiwa sh 50 milioni na shule itakayopanda miti 1500 na kuitunza kwa asilimia 80 itazawadiwa sh 30.milioni na ya tatu ni Ile shule itakayopanda miti 1,000 na asilimia 70 ikakua vizuri itazawadiwa sh. 20 million "amesema kaimu meneja wa NMB Kanda ya Dar esalaam
Naye mwakilishi wa kampuni ya Taifa Gesi ambao nao wanaendesha shindano Hilo Kwa vyomba vya habari na Kwa Halmashauri za Wilaya ,Angel Bhoke amesema kutokana na vitendo vya ukataji miti vinavyofanywa na binafamu kwa shughuli mbalinbali ikiwemo kutengeneza mkaa vimekuwa vikisababisha upotevu wa miti ekari 400,000 kila mwaka kitendo ambacho ni hatari kwa mazingira.
"Sisi kwa upande wetu baada ya kuliona hilo tukaamua kuja na mpango wa kuzishindanisha Halmashauri kuhusu upandaji miti na kwamba tutatoa zawadi kwa zitakazoshinda kutokana na vigezo tutakavyowaelekeza baadae"amesema Bhoke
Ametaja kundi lingine litakalonufaika na mashindano hayo ni upande wa waandishi wa habari nchini wa magazeti,TV na ,Radio ambapo masharti ni kuandika habari zinazotoa elimu kwa jamii ili kuongeza uelewa wa hasara zitokanazo na ukataji miti na kutambua matumizi ya nishati ya gesi kwa kupika.
"Mashindano yatafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kwa waandishi wa habari nchi nzima na baada ya hapo tutatoa zawadi na hili tunaamini itakuwa njia mojawapo ya kuelimisha jamii ili kutambua madhara yatokanayo na ukataji holela wa miti."amesema mwakilishi hiyo kampuni ya Taifa Gesi
Awali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge , Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon amesema mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa ya Tanzania ambayo iliathiriwa na ukataji miti lakini kwa sasa wameendelea kufanya jitihada za kurejesha kwenye hali yake kwa kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali.
"Mpaka sasa tumepanda miti 9.7 milioni na tumeendelea kupanda na hii ni moja ya mkakati ambao tumejiwekea ili kurejesha uoto wa asili"amesema
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Dk Selemani Jaffo ameuagiza uongozi wa kampuni ya Taifa Gesi kuzifungia mitambo ya gesi shule za sekondari za bweni na pia waende kwenye taasisi wazungumze nao namna ya kulipana ili ziachane na matumizi ya kuni kwa kupikia.
"Utafiti unaonyesha matumizi ya gesi gharama yake iko chini ukilinganisha na kuni mfano shule ya Sekondari Ruvu kabla ya kuanza matumizi ya gesi walikuwa wanatumia sh.4 milioni kwa mwezi lakini kwa kutumia gesi waliyounganishiwa na Taifa Gesi sasa wanatumia sh 2 milioni kwa mwezi"amesema Dokta Jafo.
Post A Comment: