Na Denis Chambi,Tanga.
Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete ameliagiza shirika la Reli Tanzania mkoa wa Tanga kuhakikisha ikarabati kipande cha reli kinachotoka kituo kikubwa cha Mkwakwani hadi bandari ya Tanga hii ikilenga hasa kuongeza kasi ya usafirishaji wa mizigo inayotoka na kuingia katika bandari hiyo.
Alitoa
maagizo hayo april 1,2023 mara baada ya kutembelea mradi wa ukarabati katika bandari hiyo ambapo kwa sasa umefikia asilimia 98.9 katika utekelezaji wake
ikiwa ni uboreshaji wa gati 2 kutoka urefu wa kilomita 1.7 hadi
kilomita 450 pamoja na kuongeza kina cha bandari kutoka mita 3 hadi 13
mradi wote ukigharimu jumla ya shilingi Billion 429.1 zilizotolewa na
serikali.
Mamlaka ya
Bandari ambayo ilikiri kupokea mapendekezo hayo ya ukarabati wa kipande
hicho cha reli hivi karibuni kutoka shiria la reli ilieleza mbele ya naibu waziri kuwa itakaa na ndani ya
wiki moja na kutoa majibu ya ukarabati huo huku Naibu waziri
akizipunguza siku hizo na kuwaagiza ndani ya siku tatu kuja na majibu
kamili ya nini kifanyike ili kuweza kukamilisha mradi huo.
Hata
hivyo shirika la reli ambalo limeshapeleka mapendekezo ya gharama
kwaajili ukarabati wa kipande cha reli hiyo kinachotoka kituo kikubwa
hadi bandarini hapo tayari TPA wameshatenga kiasi cha shilingi
Million 500 kwaajili ya kazi hiyo.
"Nimewapa
maelekezo watu wa Reli kwamba walichelewa kuleta mapendekezo kwa
mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Bandari wana fedha kwaajili ya zoezi
hilo na wamesema ndani ya wiki moja watakuwa wameshazipitia ili watu
wa reli waanze kufanya hiyo kazi na mimi nimesema sio wiki moja, wiki
moja ni mbali fanyeni ndani ya siku tatu muwe mmeshawarudishia majibu
watu wa reli ili waanze kuihuisha reli iliyokuwepo zamani ndani ya
bandari hii ya Tanga" alisema Mwakibete.
Uboreshaji
wa bandari hiyo umeanza kuzaa matunda kwani kwa kipindi cha mwezi
january hadi march 2023 wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi
billion 5 ikivunja rekodi zaidi ya kupokea meli kubwa ambapo hivi
karibuni ilipokea Meli Metsovo iliyotokea nchini Marekani yenye ukubwa
wa Mita 189.9 ikiwa imebeba malighafi zinazotumika viwandani pamoja na
meli nyingine mbili ambapo awali hazikuweza kufika kutokana na kina
kidogo cha Bandari hiyo.
Awali akizungumza Mhandisi kutoka shirika la Reli "TRC' Patience Karumuna
alisema
kuwa mara baada ya kupokea maagizo kutoka kwa Makamu wa Rais Philipo
Mpango mwishoni mwa Mwaka jana walifanya usanifu wa kujua mahitaji ya
kipande hicho kinachoenda bandarini ambapo walifanikiwa kukamilisha na
kuikabidhi mamlaka ya Bandari ya Tanga.
"
Baada ha kupokea maagizo kutoka kwa makamu wa Rais ilikuwa mwezi
December upande wa shirika tukishirikiana na TPA hatua za kwanza
kabisa tulizofanya ni kurudishia miundombinu ya reli upande wa stesheni
na tumekamilisha , kwa upande wa Bandari tumeleta wasanifu wakaja
tukaangalia mahitaji yaliyopo kwa sasa hivi tukatengeneza makisio ya
gharama ambalo nalo tumelikamilisha tumeikabidhi mamlaka ya Bandari
'TPA' kwaajili ya wao waweze kulipitia "alisema Karumuna
Akizungumza
kaimu Meneja wa bandari ya Tanga Petter Milanzi aliishukuru serikali
kwa uwekezaji na maboresho makubwa hayo yaliyofanyikia ambayo sasa
matunda yake yanaonekana huku akiwakaribisha wadau na wafanyabiashara wa
ndani na nje ya nchi kuitumia bandari hiyo.
"Sisi
kama Bandari tunatoa wito kwa wadau wetu wote na watumiaji wa bandari
kwamba bandari ya Tanga imeshafunguka tupo tayari kuwahudumia na kutoa
huduma bora , tumeshajiandaa kukabiliana na ushindani ili kuweza
kuwahudumia wateja wetu vizuri, tunajua serikali imewekeza fedha nyingi
kwahiyo fedha zile zilizowekezwa lazima zitoe faida hivyo sisi kama
bandari ya Tanga lazima tutoe uhakika kuwa tupo tayari kufanya kazi ili
bandari hii iwe inaleta faida kubwa kadiri ya kilichowekezwa" alissma
Milanzi.
Kaimu meneja wa bandari Tanga Petter Milanzi akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete wakati alipofanya ziara ya yake ya siku moja kutembelea mradi unaoendelea katika bandari hiyo april 1,2023.
Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete akipata maelezo kutoka kwa mhandishi wa shirika la Reli Patience Karumuna kuhusu miundombinu ya reli ambayo inatakiwa kufika bandarini hapo ili kuzidi kurahisisha usafirishaji.
Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete akipata maelezo kutoka kwa meneja wa mradi wa Rafael Angulo Niras Resident wanaotekeleza mradi katika bandari ya Tanga ambao mpaka sasa wamefikisha asilimia 98.9.
Post A Comment: