Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Ally Hamis
mwenye umri wa Miaka 48 amekutwa amejinyonga hadi kufa ndani ya Nyumba yake
katika kijiji cha Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza na Misalaba Blog, Mwenyekiti wa kijiji cha
Itwangi Bwana Kisendi Lubinza ambaye amesema tukio hilo limetokea April 8,2023 majira ya asubuhi baada ya
familia kumkuta marehemu amejinyonga ndani ya Nyumba yake.
Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa marehemu Ally Hamis ameacha
wosia ambapo ameandika ujumbe kwa kuorodhesha gharama ya madeni anayodaiwa huku
akiwaomba ndugu zake kuyalipa madeni
hayo.
“Muda
was aa nne asubuhi nilipata taarifa kuwa Ally Hamis amejinyonga kwanza
sikuamini badaye akanipigia Mheshimiwa Diwani ikabidi niende kwenye hiyo
Familia ni kweli nikalikuta tukio hilo nilipouliza wakasema tayari wameshatoa
taarifa kituo cha Polisi”.amesema Mwenyekiti wa kijiji Bwana
Lubinza
“Kuna
wosia ameandika na ameorodhesha madeni yake yote akasema ndugu wasiache
kuyalipa aliandika deni la Baskeli yake alikuwa anadaiwa elfu arobaini (40000),
kuna Baba yake mdogo alipwe laki tatu na mwingine alipwe debe moja la Mahindi
badaye kwenye wosia wake akasema kwamba ‘nimeamua kujiua mimi mwenyewe
asishikiliwe mtu yoyote nimeamua kwa moyo wangu, nimeamua kumfuata Mama yangu
aliyetangulia mbele za haki miaka mingi iliyopita”.amesema
Mazishi ya marehemu Ally Hamis yamefanyika leo jioni
mahali alipozaliwa katika kijiji cha Itwangi
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo Mwenyekiti Bwana Kisendi Lubinza ametumia
nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa kijiji cha Itwangi kuacha tabia hizo za
kuchukua maamuzi magumu na badala yake wanapaswa kufikisha changamoto kwenye
uongozi wa kijiji ili kuona namna bora ya kutatua.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP
Janeth Magomi amethibitisha juu ya tukio hilo kuwa Ally Hamis amefariki Dunia
kwa kujinyonga chumbani kwake katika kijiji cha Itwangi Halmashauri ya Wilaya
ya Shinyanga.
“Ni kweli mtu huyo alijinyonga na akaacha ujumbe kuwa anamadeni kwahiyo askari wameshaenda wakakagua eneo la tukio walikuwa na daktari mwili umefanyiwa uchunguzi na walikabidhiwa ndugu”amesema ACP Magomi
Post A Comment: