Na John Walter-Manyara
Mrara Fc ya Mjini Babati imenyakua Kombe la Polisi Jamii Cup 2023 mkoani Manyara baada ya kuifunga Soldiers Boys ya wilayani Hanang’ mabao 2-0 katika fainali zilizopigwa uwanja wa Kwaraa mjini Babati.
Nyota wa
mchezo ni kipa wa Mrara Fc Ramadhani Nyanda ambaye hakuruhusu bao hata moja,
amekabidhiwa shilingi elfu 2 huku mwenyekiti wa UVCCM Babati mjini Magdalena
Urono akimpatia elfu 30 ahadi aliyoitoa kwa kipa ambaye hataruhusu bao hata
moja.
Aidha
mwenyekiti huyo aliaahidi kununua kila bao kwa shilingi elfu 10 ambayo imeenda
kwa wafungaji wa Mrara Fc John Pengo aliyefunga dakika ya 41 na Aidan Haidari
aliyefunga dakika ya 50.
Mshindi wa
tatu ni Sanu Fc ya Mbulu iliyoshinda kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Magugu
Rangers ya Babati.
Mbali na kukabidhiwa kombe, Mrara Fc
pia walikabidhiwa jezi, mpira na shilingi laki saba taslimu na mgeni rasmi mkuu
wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere.
Pia mdhamini wa mshindano hayo Mati
Super brands Ltd kupitia kinywaji cha Tai Original, Paa kibabe wamekabidhi
zawadi mbalimbali kwa timu zilizoshika nafasi ya pili na ya tatu.
Awali akizungumza katika
mashindano hayo kamanda wa polisi mkoa wa Manyara George Katabazi amesema lengo la Polisi jamii ni kuimarisha
mahusiano baina ya wananchi na Jeshi la Polisi jambo ambalo limefanikiwa.
Mkuu wa mkoa wa Manyara
Charles Makongoro Nyerere amewataka wananchi wawe na tabia ya kufanya mazoezi
mara kwa mara ili kuweka afya zao vizuri na kuepuka maradhi.
Viongozi wengine waliokuwepo
uwanjani hapo kushuhudia faina hizo ni Pamoja na Mkuu wa wilaya ya Hanang’
Janeth Mayanja,Katibu tawala mkoa wa Manyara Carolina Mthapula na Mwenyekiti wa
UVCCM Babati mjini Magdalena Urono.Wananchi waliojitokeza kushuhudia fainali ya michuano ya Polisi Jamii Cup mwaka 2023 katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati. Katikati ni mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere akitoa neno kwa wachezaji kabla ya fainali kati ya Mrara Fc na Soldiers Boys katika fainali iliyopigwa uwanja wa Kwaraa mjini Babati.
Post A Comment: