Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkurugenzi wa The BSL Investiment Company Limited na BSL Schools Tanzania Mr. Black ametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wa chuo cha ualimu Shinyanga SHYCOM kuhusu Nyanja na stadi za usahili.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa SHYCOM na kuhudhuriwa na wanachuo pamoja na baadhi ya hamasa wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

Mr. Black pamoja na mambo mengine amefundisha Nyanja na standi za usahili (Interview Skills) jinsi ya kuomba ajira kwenye taasisi za serikali pamoja na taasisi binafsi.

“Kabla hujaanza kutafuta kazi kwanza lazima ujue umesemea nini ama unauwezo wa kitu gani lakini pili jitahidi kufahamu je ulimwengu unahitaji nini kwa sasa lakini pia tunaangalia sera ya Nchini imeelekeza nini lakini pia jiulize kabla ya kwenda kutafuta ajira je unataka mkataba wa muda mrefu au muda mfupi unaweza kupewa mkataba wa Miaka kumi kumbe lengo lako ni kupata mkataba wa Miaka mitano tu”. Amesema Mr. Black

“Tunapokwenda kutafuta kazi tunakutana na kitu kinachoitwa usahili wa kazi babla ya kuingia kwenye chumba cha Interview kuna hatua tatu lazime uzingatie kabla hujaingia kwenye chumba cha usahili ufanye nini unapokuwa kwenye chumba cha usahili ufanye nini na baada ya kutoka kwenye chumba cha usahili ufanye nini”

“Interview ikitangazwa saa nne kamili hakikisha wewe unafika saa tatu kamili unapokuwa umejiandaa kwenye interview usipendeze sana lakini pia usikele sana na usiikamie sana jiamini jibu maswali yote unayoulizwa  taratibu na usipaniki maana kuna maswali mengine ya mitego kutaka kujua wewe unauwezo wa kutunza siri za taasisi au kampuni na ukiona swali hulifahamu siyo dhambi kukumbali kwamba sahamani swali hili silifahamu ila mtakaponipa nafasi kwenye hii kazi litajitahidi nifahamu”Amesema Mr. Black

Aidha Mr. Black amefundisha jinsi ya kujiajiri na uanzishaji miradi ya kielimu, utafutaji mtaji na hatua sahihi katika utafutaji ajira kwa wanachuo hao wa chuo cha SHYCOM.

Baadhi ya wanachuo wa chuo cha ualimu Shinyanga (SHYCOM) wamesema watafanyia kazi hayo yote waliyofundishwa huku wakipongeza na kuishukuru taasisi ya The BSL kwa kutoa elimu hiyo.

Mkurugenzi wa The BSL Investiment Company Limited na BSL Schools Tanzania Mr. Black ametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wa chuo cha SHYCOM na kwamba semina na mafunzo hayo ni endelevu katika Mkoa wa Shinyanga

 

Mkurugenzi wa The BSL Investiment Company Limited na BSL Schools Tanzania Mr. Black akitoa mafunzo kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha ualimu SHYCOM Manispaa ya Shinyanga.

 

Semina ya  mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wa chuo cha ualimu Shinyanga SHYCOM kuhusu Nyanja na stadi za usahili ikiendelea kutolewa na Mkurugenzi wa The BSL Investiment Company Limited na BSL Schools Tanzania Mr. Black





Share To:

Misalaba

Post A Comment: