Baadhi ya maeneo ya wakulima na wafugaji Kiteto hayaendelezwi na kufanya halmashauri kukosa mapato ya ndani hali inayochangia pia migogoro mingi ya ardhi.

Migogoro ya ardhi inafanya mapato ya halmashauri kushuka, na kwa sasa mashamba na maeneo ya ufugaji yameshindwa kuendelezwa kutokana na wakulima na wafugaji kugombana.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kiteto, John Nchimbi, amesema  baadhi ya viongozi wa vijiji wameshindwa  kutekeleza wajibu wao namkuitumia migogoro hiyo kama vyanzo vya mapato yao.

"Migogoro mingi ni ya wafugaji na wakulima lakini pia migogoro mingi ni ya watu kutoka nje ya wilaya kuvamia maeneo ya Kiteyo kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo bila kufuata taratibu, migogoro hii inapekekea mapato ya halmashauri kupungua maeneo ya mashamba na ugugaji hayaendelezwi sasa kwa sababu wananchi wanagombania lakini yote haya yanasabanishwa na baadhi ya viongozi wa Serikali za vijiji kutotekekeza wajibu wao"

Alisema ardhi ni mali ya Kijiji viongozi na Serikali zao za vijiji wanatakiwa kufuata taratibu katika utoaji na urasimishaji wa ardhi hiyo na  kutofuata utaratibu huo ndio kunapelekea migogoro hiyo, amesema Nchimbi

Amesema pamoja na changamoto ya migogoro hiyo, kwa miaka ya hivi karibuni migogoro hiyo imepungua sana kwa kazi kubwa inayoendelea kuifanya na Mkuu wa Wilaya ya kiteto katika kuishughulikia lakini hawezi kuimaliza yote km zaidi ya ekfu 16 za mraba

"Wananchi msiuze ardhi ambazo sio zenu, viongozi msiuze ardhi na kurasimisha bila kufuata taratibu za kisheria, lakini pia hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wanaovunja taratibu kwa sababu ardhi hii ni ya wanaKiteto lazima itumiwe kwa faida ya wote"alisisitiza Nchimbi

"Ardhi hii sio kwa kundi flani la wakulima au kundi flani la wafugaji kila mtu ajione ana sababu ya kuendelea kuwa na ardhi na hili tatizo limekuwa kibwa sana sasa hivi imefikia vijiji vingi havimiliki kabisa ardhi mfano Kijiji cha Napilkunya"

Alisema Kijiji hicho kimepata sh 101mil kwenye bomba la mafuta kwa ajili ya kujenga Zahanati lakini mpaka sasa tunavyoongea Kijiji kimeshindwa kupata eneo hilo hilo kwa sababu ardhi yote wamegawa na kuuza kwa watu wengine hawakubakisha hata pori moja kwa ajili ya maisha yao ya baadaye

"Natoa rai kila kijiji kihakikishe kuwa na eneo kwa ajili ya maendeleo yake ambayo watahifadhi baada ya kupitisha kwenye mikutano yao kwamba eneo hilo haliwezi kuuzwa tena ama kugawiwa kwa namna yoyote ile, tushirikiane katika usimamizi wa ardhi hii na kila mmoja akitekeleza wajibu wake tutafanikiwa kuondoa migogoro ya ardhi Kiteto"

Kwa upandewa wananchi akiwemo Rajabu Musa mkazi wa Kaloleni amesema kesi nyingi mahakamani na kwenye mabaraza ya ardhi zinahusu migogoro ya ardhi hali inayo chelewesha maendeleo wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Kiteto Hassan Losioki akiwa eneo la Olengasho Kijiji cha Kimana amesema, kama hawatomaliza migogoro hiyo kipindi hicho wakulima wakianza  kilimo wasisumbuliwe na waendelee na shughuli zao.

"Tumekubaliana kutembea maeneo yote ya malisho ambayo yanalalamikiwa na wafugaji kuwa yamevamiwa na wakukima...lakini tukiri kuwa uchunguzi uliofanyika maeneo mengi sana ya malisho yanalimwa na wafugaji wenyewe, lakini pia tumebaini maeneo mengi ya malisho yameuzwa na wafugaji wenyewe"

Alisema ikibainika mfugaji amelima eneo la malisho ataliachia eneo hilo bila fidia yoyote lakini pia ikibainika eneo la malisho limeuzwa na mfugaji Serikali itaelekezwa isimamie zoezi hilo na kuhakikisha mfugaji amlipe gharama mkulima ili akatafute shamba jingine aliachie eneo la malisho libaki wazi alisema Losioki 

Alisema wakibaini eneo la malisho limeuzwa na kiongozi wa Serikali ya kijiji Serikali ichukue eneo lake akabidhiwe aliyeuziwa eneo la malisho ili aliyeuziwa abaki salama na eneo la malisho libaki salama.


Share To:

Post A Comment: