Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa habari wa Iringa juu ya matukio mbalimbali yaliyojitokeza mkoa humoMoja Kati ya silaa zilizokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa Iringa.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Amani Martin mkazi wa kata ya Nzihi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa mwaka mmoja na kumsababishiam makali
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumshika mtoto kwa nguvu na kumfanyia kitendo hicho wakati wakiwa shambani baada ya mama wa mtoto kuondoka kwenda kuokota kuni na kumuacha mtoto akiwa na baba yake
Kamanda Bukumbi amesema kiini cha tukio hilo bado kinachunguzwa na mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.
Aidha Jeshi la Polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa watatu kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume na utaratibu katika maeneo tofauti ya mkoa huo huku baadhi yao wakikodisha silaha hizo kwa watu kinyume na sheria.
Post A Comment: