Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile akiwaambia wananchi wa Kijiji cha Mchangani namna ambavyo atatua changamoto ya mawasiliano ya simu katika Kijiji hicho.
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile ameahidi kutatua changamoto ya mawasiliano ya mtandao wa simu katika Kijiji cha Mchangani kata ya Stesheni ili wananchi waweze kupata mawasiliano kwa urahisi.
Akijibu maombi ya wananchi wa Kijiji cha Mchangani, mbunge Dkt Chinguile alisema kuwa amepokea changamoto ya kukosekana kwa mawasiliano ya mtandao wa simu hivyo ataenda bungeni kupambana ili kuhakikisha wananchi wapata mawasiliano katika maeneo yao.
Dkt Chinguile alisema kuwa atauliza swali moja tu bungeni ni namna gani serikali itatua changamoto ya mawasiliano katika Kijiji cha Mchangani na wananchi watapata majibu husika kwa kuletewa mtandao wa simu ambao hautasumbua.
Aliwaambia wananchi wa Kijiji cha Mchangani wasiwe na wasisi watapata mtandao wa simu ambao hautasumbua kwenda kuongea na simu mbali na eneo husika.
Awali wananchi walisema kuwa wanakumbana na changamoto ya kukosekana kwa mawasiliano mazuri hadi kuhatarisha ndoa zao zao.
Post A Comment: