Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameahidi kujenga ulingo wa ngumi kwa ajili ya mabondia wa Jijini Dodoma ikiwa ni hatua ya kuukuza na kuuendeleza mchezo wa masumbwi mkoani Dodoma.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo wakati alipomtembelea bondia Laurent Segu kutoka Dodoma ambaye atashiriki katika pambano la utangulizi dhibi ya Bondia Ibrahim Najum kutoka Mbeya ikiwa ni sehemu ya pambano la utangulizi kati ya Bondia Hassan Mwakinyo dhidi ya Bondia Kuvesa Katemba kutoka Congo pambano litakalonyika Jijini Dodoma siku ya kesho Jumapili tarehe 23.04.2023
“Nimekuja leo kukutembelea kambini kwako na nimeona maandalizi yako mazuri dhidi ya pambalo lililopo mbele yako.
Ni imani yangu utalinda heshima ya Dodoma na kufanya vizuri katika mchezo huu.Ushindi wako utakuwa ni kichochea kikubwa kwa mabondia wengine wa Dodoma kufanya vizuri.
Mmekuwa na changamoto kubwa ya ulingo wa ngumi kwa muda mrefu, nataka kuwahakikishia kwamba mwaka huu nitawatengenezea ulingo ili tuuendeleze huu mchezo wa masumbwi kwa kuwa na miundombinu mizuri na pia ili kuongeza hamasa ya mchezo huu ambao miaka ya nyuma ulileta heshima kubwa sana hapa mkoani Dodoma”Alisema Mavunde
Akitoa salamu za shukrani, Bondia Laurent Segu amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kusimamia mahitaji yake na kuwa karibu naye kipindi chote cha maandalizi ya pambano hili sambamba na motisha ya ushindi ya Tsh 1,000,000 na kuahidi kufanya vizuri katika pambano hilo ili kupeperusha vyema bendera ya Dodoma katika mchezo wa masumbwi.
Post A Comment: