Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah amesema mchango wa Marehemu Sheikh Abeid Amani  Karume utaendela kuenziwa  huku Wazanzibari tukiamini kuwa ndiyo chachu ya Maendeleo kwa Zanzibar ya Uchumi wa bluu.

Mhe. Hemed amesema hayo wakati akizungumza kwenye kongamano la Tano la kumuenzi Marehemu Sheikh Abedi Amani Karume katika kampasi ya Karume, Bububu, Zanzibar.


Mhe Hemed  amesema Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kinaishi kwa Falsafa, Fikra,maono na michango ya Wasisi wa Taifa huku ikiendeleza na kutambua ndoto za Waasisis hao zinatimizwa katika Taifa la Tanzania.

"Madhila ya wakoloni yalitufanya sisi tuishi daraja la chini, natoa wito kwa vijana kusoma histori   ili kujifunza na kuishi kwa maono ya Waasisi wa Taifa letu,”alisitiza Mhe.Hemed.


Mhe. Hemed alisema kupitia makongamano ambayo Chuo kimekukwa  kikiyafanya yanasaidia vijana wetu kubadilika ki tabia, kujua historia ya taifa na falsasa za Waasisi  kwa lengo la kuandaa vijana kuwa raia wema kwa Taifa la Tanzania.

“Tumeona ubunifu wa kisasa, serikali imefarijika sana kuona jitihada zinazochukuliwa na  na Chuo hiki katika kuendeleza bunifu zenye tija na zenye lengo la kuatua changamoto mbalimbali katika jamii,”alisisitiza Mhe. Abdullah.


 Mkuu wa Chuo cha Kunbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema kongamano hili la tano ni la muhimu sana katika kutunza na kuenzi historia za Waasisi wa Taifa.
Prof. Mwakalila amesema pamoja na mambo mengine Chuo kina tekeleza masuala mbalimbali ikiwemo kutoa Mafunzo katika fani mbalimbali, kutoa Mafunzo ya Uongozi, Maadili, Uzakendo na Utaifa, Kufanya tafiti mbakimbali kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali katika jamii na kutoa ushauri  wa Kitaalamu katika jamii na sekta za Umma.

“Tangu Maonesho ya kitaifa ya Sayansi Teknolojia na ubunifu (MAKISATU) yalipoanza Chuo kimekuwa kikipata ushindi kupitia maonesho hayo, kwa kuwa na bunifu zenye tija katika jamii,”alisisitiza Prof.Mwakalila.

Profesa Mwakalila amesema kuwa, Chuo kina utaratibu wa kuandaa makongamano ya kitaaluma na kuwa kila inapofika mwezi wa Nne huwa Chuo, kinatafakari  kwa pamoja Maono na Kuenzi Waasisi wa Taifa na kuwa  hili ni Kongamano la Tano kwa Kampasi hii ya Karume lengo ni kujikumbusha Misingi aliyoijenga Mzee Karume.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mzee Stephen Wasira amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini na kumteua tena kuendeela kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo kwa kipindi cha Pili, ambapo ameahidi kufanya kazi kwa uamini ili Chuo kiweze kufikia Maelengo yake.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
4.04.2023
Share To:

Post A Comment: