MUWEKEZAJI Mzawa Mjini Singida,Leonard Suih aliyewekeza kwenye majengo amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro kati yake na Halmashauri ya Manispaa ya Singida inayomtaka kutoka na kubomoa majengo yake ya biashara.
Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dodoma juzi kwa lengo la kufikisha malalamiko yake kwa Rais,Mwekezaji huyo alieleza kuwa majengo hayo ameyajenga kwenye ardhi inayomilikiwa na Halmashauri hiyo kwa makubaliano na amedai amepewa kibali cha ujenzi.
Suih alidai kuwa ameruhusiwa kujenga katika eneo hilo na Halmashauri tangu mwaka 1995 ambapo alidai amejenga vyoo na bafu za kulipia katika eneo hilo ambapo vilikuwa vinatumika kwajili ya stendi ambayo ilikuwepo eneo hilo zamani pamoja na kupewa sharti la kujenga ghorofa ambapo tayari maandalizi ya jengo la ghorofa tatu yalikuwa yameshaanza ikiwemo kuchimba msingi na kuwekeza biashara na majengo mengine yenye gharama zaidi ya milioni 600.
Ameeleza jinsi alivyolipata eneo hilo hadi kuruhusiwa kujenga ambapo amesema eneo hilo lilikuwa na dampo kubwa lilikuwa na takataka zaidi ya tani 2000 kutokana na hayo yeye alifanya utafiti jinsi ya kuliondoa hilo dampo ili kuondoa takataka hizo zilizokuwa zinasababisha ugonjwa wa kipindupindu.
"Waandishi lile dampo lilikuwa kubwa sana,nilivyoona dampo nilifanya utafiti jinsi ya kuliondoa nikawashirikisha Manispaa ili niwaombe lile eneo kwa matumizi ya kujenga vyoo vya kulipia na bafu ,niliiomba Manispaa iondoe zile taka ili nitumie eneo hilo kwajili ya vyoo vyakulipia walikubali wakatafuta Kampuni kwajili ya kuzoa taka kampuni hiyo ikataka milioni sita kwajili kuondoa taka hizo lakini Manispaa ikashindwa hiyo gharama ikaniambia niziondoe mwenyewe taka hizo.
"Niliingia makubaliano na Manispaa hiyo kuwa nisombe kwa gharama zangu lakini watanirudishia ,hivyo niliiomba Kampuni hiyo inipunguzie ikakubali kunipunguzia nikasomba kwa shilingi Mil.2.8 badala ya milioni 6.
"Lakini Halmashauri haijanilipa hiyo fedha na badala yake niliomba kujenga katika lile eneo ilikufidia pesa niliyoondolea taka kwasababu ilikuwa kwenye makubaliano ya kunilipa na Halmashauri ikakubali na kuniruhusu kujenga na nilipewa kibali cha ujenzi.
"Lile dampo ndiyo lilikuwa chanzo cha tatizo la ugonjwa wa kipindupindu Singida , mimi niliondoa taka tani 1500 na baada ya kuondoa zile taka na kujenga vyoo pale ndugu waandishi kipindupindu kiliisha kabisa jijini Singida hadi leo kwani zile taka ndiyo zilikuwa zinasababisha kipindupindu na zilikuwa nyingi sana,"ameeleza.
Amesema kuwa baada ya yeye kujenga majengo hayo mgogoro ndipo ukaanza ambapo hadi sasa unamiaka 28 na umekuwa ukiibuka na kupoa mara kwa mara hali ambayo inasababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake kwa amani na kumuathiri kisaikojia huku akitumia gharama kubwa kwajili ya mgogoro huo.
Akizungumzia mgogoro huo Suih ameeleza kuwa.
“Siku moja nipo kwenye kikao nikapata simu ya vijana wangu wakiniambia kuwa hapa ofisini kuna watu tisa wamekuja na bunduki wanakutafuta nikahoji wananitafuta na bunduki nikashtuka sana kwa kosa gani la kunitafuta na bunduki mimi.
“Nikatoka kwenye kikao nikaenda nikakuta kweli watu hao wakiwa kwenye gari aina ya Pick up wakiwa na bunduki wakasema wameniletea notisi wakidai kuwa wanataka kuvunja majengo yangu na wakinishinikiza kusaini nikasema siwezi hadi niwasilianae na mwanasheria wangu,"ameeleza Suih.
Amesema kuwa kutokana na hali hiyo alilazimika kufungua kesi Mahakama kuu ambayo ilidumu kwa zaidi ya miaka mitano na kujikuta akiwa ametumia zaidi ya Sh. milioni 30 kuendesha shauri hilo.
“Nimekwenda na kesi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano na kutumia zaidi ya Sh. milioni 30 lakini baadae wakanifuata baadhi ya watumishi wa Manispaa na madiwani wakidai kuwa nifute kesi ile ili tuzungumze nje ya mahakama nikaona sawa nikawakubalia”amesema.
Aidha amesema pamoja na kukubali lakini amekuwa akipata vitisho na usumbufu wa mara kwa mara na kuzalilishwa na viongozi wa Manispaa na Mkoa huo ikiwani ni pamoja na kumlazimisha kusaini mkataba mpya ambao unamuondolea haki ya umiliki wa eneo hilo na majengo yake.
“Hivi juzi nilikuwa nafanya ukarabati kidogo wa kubadili paa lilikuwa limechoka akaja Mhandisi wa Manispaa na akasema nisifanye lolote nisimamishe ujenzi nikaomba basi nirudishiwe hata mabati ili bidhaa zisinyeshewe akasema hakuna kufanya lolote, matokeo yake mvua ikaharibu bidhaa zilizokuwepo na picha ninazo hapa”amesema
Ameeleza kufuatia hali hiyo alimpigia simu mkuu wa mkoa Singida na kumtumia picha za uharibifu huo na kwenda kumuona ofisini kwake lakini hakuna alichoambulia.
“Baada ya kumpigia simu aliniambia niende ofisini lakini cha ajabu kumbe tayari alishapewa maneno na mkurugenzi hata mimi nilipojieleza hakunisikiliza na kuniambia kuwa wewe unapesa sisi tuna mamlaka na ukiendelea kuongea naweza kutuma watu wakavunje hata muda huu.
“Sasa nimeamua kufunga safari kuja Dodoma kwa ajili ya suala hili kwani mgogoro huu umekuwa na sura mpya kila siku na wale viongozi tunaowategemea hawana msaada sasa kupitia vyombo vya habari naomba kilio changu mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani anisaidie kwani hajui wanayotenda wateule wake tumeona jitihada zake za kuhamasisha wawekezaji wa nje na ndani lakini kwangu ni manyanyaso kila siku”amesema
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, alipoulizwa kuhusu malalamiko hayo kwa njia ya simu amesema kuwa mkataba baina ya Manispaa ya Singida na mwekezaji huyo unamtaka kutofanya jambo lolote hadi apatiwe kibali.
“Lile ni eneo la ubia baina ya Manispaa na mwekezaji sasa hawezi kufanya kitu bila sisi kujua ili kama kunagharama ametumia tujue na mkataba wake upo mwisho unakwisha 2025 tumemwambia aandike barua lakini hataki kwanini”alihoji Serukamba
Hata hivyo, alisema kinachofanywa na Mkoa ni kwa mujibu wa mkataba ambao walikubaliana pande zote mbili lakini mwekezaji anaonekana hataki kuufuata na kufanya kinyume na makubaliano yao.
“Tulishaongea naye mbele ya mke wake akasema anakwenda kuandika barua lakini hadi leo hajaleta barua kwanini, yeye alete barua ya kuomba kibali na sisi tutampatia ruhusa ya kufanya kile anachotaka”amesisitiza Serukamba
Post A Comment: