Na,Jusline Marco;Arusha

Kesi ya jinai ya kupotea kqa mzee Oriais Oleng'iyo mwenye umri wa miaka 85 Mkazi wa Loliondo Wolayani Ngorongoro imepangwa kusikilizwa tena Mei 10 mwaka juu mbele ya hakimu Mohamed Gwae katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa inawahusu wajibu maombi sita ambao ni walalamikiwa ,Waliolalamikiwa kwa vyeo vyao akiwemo  Mkuu wa kituo cha polisi Ngorongoro ,Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro ,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Walalamikiwa hao wamepinga maombi ya mlalamikaji wa kesi hiyo yaliyo wasilishwa April 30 katika Mahakama kuu kanda ya Arusha ambapo Wakili wa Serikali anayewawakilisha wajibu maombi hao ,Peter Mseti mbele ya Jaji Mohamed Gwae amesema kwa mujibu wa kifungu cha sheria 390 kifungu kidogo cha kwanza A na B ,ni lazima mleta maombi aonyeshe kuwa na uhakika na sio kuzaniwa au kuhisiwa.

Aidha wakili huyo ameeleza kuwa mleta maombi hajaeleza wazi namba  ya gari lililombeba Mzee Oriais na pia hakutaja namba wala jina la askari aliyeonekana akimchukua mzee huyo anayetafutwa,ambapo amesema katika maombi ya mleta maombi huyo ameshindwa kuthibitisha kuwa aliyekamatwa yupo jela na kudai kuwa  Wajibu maombi hawajawai kupokea malalamiko yeyote ya mtu aliyepotea pia hawajawai kumshikilia mtu wa namna hiyo.

Mmmoja wa  Mawakili wa Mleta maombi, Joseph Oleshangai akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo amesema mleta maombi amedai kuwa  maombi  waliyowasilisha ni kuiomba mahakama iwaamrishe walalamikiwa hao kumleta Bw .Oriaisi akiwa hai au kuuleta mwili wake ama kumwachia huru au kumshtaki endapo anatuhumiwa.  

Ameongeza kuwa  Julai 09 2022 katika Kitongoji cha Nairowa Kata Ololosokwan Wilayani Ngorongoro  askari polisi walikuwa wakitoa ulinzi kwa maafisa wa serikali waliokuwa wanaweka vigingi kwenye pori tengefu la Pololeti ambapo baadhi ya wakazi walikuwa wakipinga zoezi hilo ndipo palitokea machafuko kati ya wananchi na polisi hivyo kupelekea askari kurusha risasi  za moto

Ameendelea kueleza kuwa vurugu hizo zilifanyika jirani na nyumbani kwa Bw. Oriais ambaye hakuwepo na hakuhusika kabisa katika vurugu hizo lakini alipatwa na risasi ambapo askari walikamata  baadhi ya wananchi  waliokuwa katika vurugu hizo  ambao baadaye walifikishwa mahakamani lakini mzee oriais hakuwepo  miongoni mwao ili hali na yeye alokamatwa na polisi hao.

Madai ya kupigwa risasi na kupotezwa kwa Mzee Oriais Oleng’iyo ni matokeo ya operesheni iliyofanyika Loliondo mnamo tarehe 10 mwezi Juni mwaka jana  wakati wa uwekaji vigingi katika eneo la vijiji 14 vya Loliondo lenye kilometa za mraba 1502.

Share To:

Post A Comment: