Uongozi wa umoja wa wanawake Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi UWT Mkoa wa Arusha umefanya kikao cha baraza la mkoa ili kutoa utatuzi wa changamoto walizokutana nazo katika ziara ya siku tatu iliyofanyika katika wilaya ya Arumeru mkoani humo ikiwemo sekta ya afya ,ukatil kijinsia na mikopo kwa wanawake.
Miongoni Mwa changamoto zilizotolewa fafanuzi ni pamoja na Zahanati ya kata ya Maruvango kukosa vifaa tiba na vitanda vya kujifungulia wakina mama wajawazito naseikali imekwisha andaa bajeti katika kutatua changamoto hiyo katika vituo vyote vya afya ambavyo vimekuwa na changamoto kubwa. amesema DMO Mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru Dr Maneno Focus
Pia amesema serikali unania njema na watu wake hususani kwa wakinamama kwa kuendelea kupambana na vifo vya mama na mtoto kwa kuboresha huduma bora ya afya
Afsa maendeleo ya jamii wilaya ya meru frola Msilu amewataka maafisa maendeleo ya jamii wakata kuwana ushirikiano wakutosha katika kufanya kazi huku akiwataka wakina mama ambao vikundi vyao havirejeshi mikopo kwa wakati warudishi ili wengine waweze
Ili kupinga swala la ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru imeanzisha vikundi mbalimbali mashuleni vinavyotoa elimu kwa wanafunzi itakayo saidia kupunguza ukatili wa kijinsia kwa watoto huku wakishirikiana na wazazi kiwachukukia hatua wahusika. Amesema frola Msilu.
Nae Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Mtatifikolo Kaganda ameupongeza uongozi wa UWT kwa kazi wanazozifanya kwa manufaa ya wananchi huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizotolewa na wananchi kufikana na fedha zilizotolewa na serikali katika sekta ya Elimu bilion moja na million miasaba arobaini, afya bilioni mbili na milioni miasaba na mikopo isiyo nariba bilioni moja na milioni mia moja sabini na sita.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Flora Zelothe akiwa Mgeni rasmi katika baraza hilo amezungumzia swala la ukatili linazidi kukua Siku baada ya Siku hivyo juhudi zi nahitajika.
"Ukatili wa kijinsia Umekuwa ukifanyika asilimia 66.6 majumbani hii inatokana na wamama kuwa bize na kutafuta kipato mda mwingi wanakuwa makzini na katika biashara wakirudi nyumbani usiku wakiwa wamechoka nakupelekea kukosa mda wa kumkagua mtoto wake.
Pia amewataka wanawake kuhamasishana kugombea nafasi mbalimbali katika uongozi ili kufanikisha jambo hilo ni lazima wanawake wawe na umoja kwa kushikamana na kupendana.
Nae mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Juliet Maturu ameushukuru uongozi wa mkoa kwa kutembelea katika wilaya yake na kuwataka viongozi wa ngazi zote kuanzia vijiji mpaka tarafa kufanya kazi kwa kushirikiana na kujitoa.
Post A Comment: