Na Christina Thomas,Kilosa, Morogoro.
ZAIDI ya Kaya 750 katika kijiji cha Mambegwa wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro wanakabiliwa na jangwa la njaa kutokana na mabadiriko ya tabia ya Nchi na kusababisha mazao yao kukauka kutokana na ukame uliojitokeza sehemu mbalimbali nchini ambapo wameiomba Serikali kuona haja ya kuwasaidia vyakula vya gharama nafuu.
Hali hiyo imeonekana wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kilosa, ambapo mazingira halisi ya kijiji hicho inaonesha mabadiliko ya tabianchi yameathiri mazao ya wakazi hao ambapo mazao mazao yao shambani yameungua pamoja na vyanzo vya maji kukauka.
'Tumelima na kupanda mazao haya mwezi wa kumi na mbili matarajio yetu yalikuwa kuwa mwezi huu tuanze kuona mazao tutakayovuna lakini hali ni mbaya jua limekuwa kali mazao yameungua na sasa hatuna chochote tunaomba serikali ituletee hata mazao ambayo yatauzwa kwa bei ya chini kwani huku kwa sasa sado ya lita nne ni shilingi 8,000' alisema Twalib Ngonjani Mkazi wa kijiji cha Mambegwa.
Ongezeko la mifugo limetajwa kuchangia kwa kiasi uharibifu wa mazingira ambapo baadhi ya viongozi wanatajwa kutokuwa waaminifu katika usimamizi wa mifugo inayoingia katika eneo hilo 'Viongozi wengi huwa hawana desturi ya kuja kututembelea sasa uchaguzi unakaribia ndio wanakuja kututembelea, wapo pia viongozi ambao sio waaminifu wanashindwa kusimamia wafugaji na wanasababisha mifugo yao kutuharibia mazingira' alisema Sefu Makubi Mkazi wa Kijiji cha Mambegwa.
Ombi kubwa la wakazi wa Kijiji hicho kwa Serikali ni kuona namna ya kukikomboa kijiji hicho na janga la njaa ambalo wanaweza kukumbana nalo kutokana na mazao yao mengi kukauka kwa ukame ambao umetokeza kwa msimu huu wa kilimo huku gharama za vyakula zikiwa juu.
Kwa upande wake katibu wa umoja wa vijana chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kilosa Nyansio Gregory ametoa wito kwa watendaji wa vijiji kutoa taarifa za uwazi ili Serikali iweze kuchukua hatua madhubuti kwa wakati.
'Tumetembelea huku ambako ndio chanzo cha uzalishaji wa mazao ya chakula tumeona hali ni mbaya wananchi wetu mazao yao yameharibika, sasa ni lazima watendaji wetu wa vijiji watoe taarifa za uwazi ili watusaidie sisi chama na serikali kutambua changamoto hizi ili ziweze kushughulikiwa mapema, wananchi wetu wanateseka sana' Amesema Nyansio Gregory, Katibu waumoja wa Vijana CCM wilaya ya Kilosa.
Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi baada ya kupokea changamoto hizo, akakemea vikali tabia za wananchi kuharibu mazingira na na kuahidi kufikisha changamoto hiyo katika mamlaka husika na kamati za maafa.
'Sisi tusijione ndio wa mwisho kuishi sisi sio wa mwisho, kuna familia zitakuja kuishi hapa na mazingira tumeyaharibu sasa wataishije hapa, hili kwetu ni pigo njee ya yale kumi ambayo mungu aliipiga Dunia, hili liwe ni fundisho kwetu ili tusiharibu mazingira, kwa sababu haya yametokana na uharibifu mkubwa wa mazingira Amesema Prof. Kabudi.
Post A Comment: