Na Okuly Julius-Dodoma
Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imesema mifumo wanayoitengeneza inalenga kuleta suluhu katika matatizo na kupunguza gharama zinazotumika kutekeleza shughuli mbalimbali za serikali.
Hayo ymeelezwa na Afisa TEHAMA wa Mamlaka hiyo Tumaini Masinsi ,wakati akizungumza na waandishi wa habari,waliotembelea katika Banda la e-GA lililopo katika Maonesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma,leo Aprili 28,2023.
Ambapo Masinsi amesema kuwa wanapambana kuhakikisha mifumo yote muhimu inatengenezwa na inafanya kazi ili kuendelea kuiunga mkono serikali katika jitihada za kuhakikisha sayansi,teknolojia na ubunifu unatumika kwa faida na kuongeza uchumi wa taifa.
"Tunachokifanya ni kuhakikisha tunaleta suluhisho katika matatizo na kupunguza gharama zinazotumika kutekeleza shughuli mbalimbali za serikali na Taasisi zake kwa kubuni mifumo wezeshi ambayo inarahisisha muda na inafanyika kwa ufanisi mkubwa,"
Na kuongeza kuwa "tunaishukuru Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuandaa wiki hii ya ubunifu kwani imesaidia kuwaleta pamoja wabunifu kupitia taasisi zao na sisi kama eGA tumepata nafasi ya kuonesha bunifu zetu mpya ambayo tayari zimeanza kufanya kazi na zimesaidia kuboresha utendaji katika sekta mbalimbali hapa nchini,"amesema Masinsi
Maonesho ya wiki ya Ubunifu Tanzania mwaka 2023 yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kushirikisha ni Taasisi za Elimu ya Juu, Taasisi za Utafiti na Maendeleo, Vyuo vya Ufundi, Mashirika na Taasisi za Umma, Mashirika na Taasisi binafsi za teknolojia, Wizara mbalimbali na Wabunifu walioendeleza katika programu ya MAKISATU na kufikia hatua ya ubiasharishaji.
Lengo likiwa ni kuwakutanisha wabunifu mbalimbali ambapo wanatumia maonesho hayo kama jukwaa la kuonesha bidhaa zao mpya ambazo wamezibuni kupitia Taasisi zao ili jamii ione na kuvichukuwa kwa ajili ya kwenda kuvitumia kwa kutatua changamoto zao na kurahisisha utendaji katika shughuli za kila siku.
Zifuatazo ni Mifumo nane mipya ambayo imetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kutumia wataalamu wake wa ndani q na zimeanza kufanya kazi.
Ni mfumo wa kuratibu shughuli za kimawasiliano kwa kupiga simu kwa Taasisi mbalimbali za Umma.
Mfumo huu ni mahususi kwa ajili kuongeza ufanisi wakuhudumia wananchi wenye malalamiko, maulizo mapendekezo, na pongezi
2.ChatAI
Ni ubunifu unaotumia teknolojia ya akili bandia kusaidia Mamlaka ya Serikali Mtandao kujibu maswali ya mara kwa mara kuhusiana na utendaji kazi wa Mamlaka. Mfumo huu unapatikana kupitia ega.bot.all.co.tz
3.Alphachain Blockchain Network
Ni ubunifu wa ndani wa mtandao wa blockchain unaohimiza matumizi ya mtandao wa blockchain kutengenza mifumo mbalimbali.
4.Sec doc
Ni ubunifu wa mtandao unaotokana na teknolojia ya blockchain yenye malengo ya kuongeza ulinzi kwenye matumizi na utumaji wa nyaraka mbalimbali.
5.eMrejesho
Ni mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi kwenda kwa taasisi mbalimbali za umma. Mfumo huu unapatika kwa njia ya web “eMrejesho.gov.go.tz” njia ya mobile application kwa Playstore na Applestore kwa jina la mrejesho pia kwa njia ya msimbo *152*00# kisha namba 9, kisha namba 2.
6.EBoard
Ni mfumo wa kuratibu vikao vya bodi na kamati zake, menejimenti na kamati zake pamoja na madiwani.
Mfumo huu umekua suluhu kubwa katika kupunguza gharama za utendaji kazi kwenye eneo hili la vikao.
7.Oxygen
Ni ubunifu wa mtandao wa kijamii wenye usalama wa hali ya juu ulioundwa kwa lengo la kufanya mawasiliano kwa message, voice calls pamoja na video calls. Mtandao huu unapatikana kwa njia ya web na mobile application kwa android na IOS.
8.RSS
Ni ubunifu wa teknolojia unaofanania na TeamView na Anydesk, unaruhusu ku share skrini za kompyuta kwa watu walio kwenye maeneo tofauti ya ki jeographia, pia unaruhusu utumaji na upokeaji wa ma faili mbali mbali kwa njia ya kielectroni.
Post A Comment: