Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile akiongea kwa furaha na wananchi wa Kijiji cha Mchangani kata ya Stesheni baada ya kutatua changamoto za maji na barabara
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile alipokuwa akiongea na wananchi hao



Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile amefanikiwa kutatua changamoto ya maji na barabara kwa wananchi wa Kijiji cha Mchangani iliyokuwa imedumu toka Tanzania kupata Uhuru.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge huyo, wananchi walisema kuwa wanampongeza sana mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile kwa jitihada za kutatua changamoto za wananchi waliompa kura.

Walisema kuwa walikuwa wanatatizo kubwa la kukosa maji Safi na salama katika Kijiji hicho na kupeleka kuamka usiku kwenda kutafuta maji umbali mrefu na kufifisha shughuli za kimaendeleo kupeleka migogoro ya ndoa ila kwa sasa ardha hiyo haipo na Wananchi wote wanafuraha.

Aidha Wananchi hao walisema kabla ya kutatua changamoto ya barabara kulikuwa hakuna gari lolote lilokuwa linafaika Kijiji cha Mchangani kata ya Stesheni.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dkt Amandus Chinguile alisema kuwa anafanya kazi ili kuhakikisha wananchi wapata maendeleo kwa wakati ili kuijenga Nachingwea mpya na ya kisasa.

Dkt Chinguile aliwataka wananchi kuwapuuza wanasiasa wote wanaoeneza habari mbaya na za uongo kuhusu mbunge huyo kuwa viatu vya kuliletea maendeleo Jimbo hilo havimtoshi.


Mbunge Dkt Chinguile aliwahidi wananchi wa Kijiji cha Mchangani kata ya Stesheni kuwatatulia changamoto zilizobaki ili ikifika kipindi cha uchaguzi asiwe na maswali ya kuulizwa kutokana na kazi kubwa ya kimaendeleo aliyoifanya jimboni.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: