Mbunge wa Jimbo la Nachingwea DR Amandus Chinguile akiongea na wananchi wa kata ya Stesheni juu ya miradi na namna ambavyo atatua kero za wananchi wa Jimbo hilo
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mchangani wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la Nachingwea DR Amandus Chinguile juu ya faida ya kuwa na kiwanda cha kubangua korosho wilaya ya Nachingwea.
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
MBUNGE wa Jimbo la Nachingwea Dkt. Amandus Chinguile ametaka kufufuliwa kwa kiwanda cha kubangua korosho alichopewa mwekezaji katika wilaya ya Nachingwea ili kuongeza thamani ya zao la korosho.
Akizungumza wakati wa ziara ya kuwatembelea wananchi wa Jimbo la Nachingwea katika Kijiji cha Mchangani kata ya Stesheni, Dkt Chinguile alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imepanga kufufua viwanda vyote vya kubangua korosho na katika Jimbo la Nachingwea kiwanda hicho kipo.
Dkt Chinguile alisema kuwa mwekezaji aliyepewa kiwanda cha kubangua korosho kilichopo Jimbo la Nachingwea amegeuza kuwa ghala la kuhifadhia mazao Jambo ambalo kinyume na makubaliano.
"Tulimpa mwekezaji ili aendeshe kiwanda cha kubangua korosho,Sasa yeye ameweka limekuwa ghala la kuhifadhia mazao kwa lugha nyepesi wananachingwea tumedanganywa" alisema Dkt Chinguile
Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan iliwatuma nje ya nchi kwenda kuangalia soko la korosho lipoje na walikuta kilo moja ya korosho iliyobanguliwa inauzwa kiasi cha shilingi elfu 80 wakati Nachingwea inauzwa elfu 20.
Hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lazima kufufua viwanda na kuanzisha viwanda vipya vya kubangua korosho ili kumuongezea thamani mkulima wa korosho wa Nachingwea.
Post A Comment: