Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa, Dkt Tumaini Msowoya amewakumbusha wahitimu wa  ualimu kutunza maadili ya taaluma yao kazini



Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa, Dkt Tumaini Msowoya amewakumbusha wahitimu wa  ualimu kutunza maadili ya taaluma yao kazini 


Dkt Msowoya alikuwa mgeni Rasmi katika Mahafali ya Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki wanaosoma Chuo Cha Ualimu cha Kleruu, Manispaa ya Iringa.


"Mnaenda kuwafundisha watoto huko shuleni tafadhali katunzeni maadili ya kazi yenu ya kazi, mkawe na nudhamu, mcheni Mungu na mkafanye kazi kwa bidii," amesema Dkt Msowoya.


Amewashauri Wanafunzi wanaobaki wasiige mikumbo badala yake wafuate masomo yaliyo waleta chuoni.


"Wanafunzi baadhi yenu mmeoana ndoa za Siri, wazazi hawajui kama huku mnaishi na ndoa zisizo rasmi, mapenzi yapo mtayakuta tu, wekezeni kwenye elimu," amesisitiza.


Wanafunzi 26 wa kike na kiume walio lelewa katika misingi ya Kanisa Katoliki wamehitimu masomo yao na wanatarajia kuanza mitihani Mei 2, 2023.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: