Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro (kulia) akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba, Magharibi Dk.Mwigulu Nchemba baada ya kuwasili kwenye Baraza la Eid lililofanyika Kijiji cha Mgunga Kata ya Mtoa wilayani Iramba mkoani Singida jana. Nchemba alikuwa mgeni rasmi katika baraza hilo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, amewataka wazazi na viongozi wa dini kutilia mkazo katika kulea vijana kwenye misingi impasayo mwenyezi Mungu na wao wakiishika hawataicha na wala hawatapitiwa na wimbi la ushoga.

Dk.Mwigulu ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi, alisema hayo jana kwenye Baraza la Eid lililofanyika katika Kijiji cha Mgunga Kata ya Mtoa wilayani Iramba mkoani Singida. 

Alisema pamoja na  hatua za kisheria zinazochukuliwa kwa wahusika lakini jambo la msingi kabisa ni kuweka mkazo katika suala la maadili.

"Tutakata matawi lakini kama shina na mizizi ipo matawi yatakuwa yanachipuka tu, tuchimbue mizizi tuondoe na shina na msingi wake upo kwenye kuwekeza kwenye maadili," alisema.

Kuhusu suala la uchumi, alisema pamoja na dunia na nchi yetu kupitia kwenye misukosuko ya kiuchumi na majanga lakini Tanzania haijayumba kutokana na uongozi  wa  Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Dk Mwigulu alisema  hakuna miradi ya maendeleo iliyokwama iwe midogo au mikubwa na haya yote yanafanyika kutokana na uimara wa Rais Samia na hivyo wananchi wa dini zote waendelee kumuombea.

Alisema mafanikio ambayo Tanzania inayo hadi nchi nyingine za Afrika zinashangaa na kujiuliza nchi zao zimekosea nini.

"Mambo haya ukiyaona yamekuwa mepesi si kwamba ni mepesi ni vile mzigo mzito ukibebwa na mwenye nguvu huanza kuonekana mwepesi," alisema.

Katika hatua nyingine Dk.Nchemba alimpongeza msaidizi wake wa dini ya kiislam jimboni humo, Shabani Sajilo kwa kuwa mchapa kazi mzuri na muaminifu kwani kila anapomtuma kutekeleza mambo kadhaa ya dini hiyo ikiwemo ujenzi wa misikiti amekuwa akitekeleza kwa haraka.

"Jimbo la Iramba Magharibi kuna vijana wengi ambao naweza kuwatuma lakini huyu Shabani amekuwa ni mwepesi kutekeleza yote ninayomtuma na nimuaminifu sana hana ujanja ujanja wala konakona" alisema Nchemba.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, aliishukru serikali wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani bei za vyakula na nguo havikuuzwa ghali na wala hakukuwa na mfumuko wa bei.

Aidha, Sheikh Nassoro aliiomba serikali kutoteteleka katika msimamo wake juu ya suala la ushoga na kushukru hatua ziluzoanza kuchukuliwa kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga.

"Nazipongeza serikali kutokana na hatua zilizoanza kuchukuliwa kupitia mahakama kwa kuanza kuwahukumu baadhi ya watu wanaojihusisha masuala ya ulawiti na ushoga na hatua hizi zisiishie kwa mashoga bali pia ziende kwa mabasha," alisema.
Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba, Magharibi Dk.Mwigulu Nchemba akizungumza na Waislam kwenye Baraza la Eid lililofanyika Kijiji cha Mgunga Kata ya Mtoa wilayani Iramba mkoani Singida jana. Nchemba alikuwa mgeni rasmi katika baraza hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba, Magharibi Dk.Mwigulu Nchemba akizungumza na baadhi ya viongozi wa Kiislam kabla ya kuanza kwa baraza hilo.
Mbunge wa Makete, Festo Sanga akizungumza kwenye baraza hilo.
Diwani wa Kata ya Mtoa, akizungumza kwenye baraza hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba, Magharibi Dk.Mwigulu Nchemba akiwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam kabla ya kuanza kwa baraza hilo.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro (kulia) na Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba, Magharibi Dk.Mwigulu Nchemba wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye baraza hilo.
Baraza likiendelea.
Waumini wa kiislam wakiwa kwenye baraza hilo.
Baraza likiendelea.
Msoma Qulaan Chipukizi Faudha Hamisi akisoma Qulaan kwa umahiri mkubwa katika baraza hilo.
Msaidizi wa Mbunge Dk. Nchemba katika Dini ya Kiislam, Shabani Sajilo, akizungumza kwenye baraza hilo.
Taswira ya baraza hilo.
 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: