Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile ameungana na Waumini zaidi ya 500 katika Msikiti mkubwa Kata ya Mkoka, Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma katika Iftari na Dua Maalum ya  kuiombea Nchi na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 Kabla ya Dua hiyo Mhe. Mbunge alitembelea Shule ya Msingi Mkoka Kitengo Maalum cha Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu(walemavu) na kuwapelekea sadaka, vitabu, kalamu na mahitaji ya shule mbalimbali. 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.










Share To:

Post A Comment: