Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Comred Daud Yassin ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Iringa na wapenzi wa michezo waendelee kujitokeza kuichangia Timu ya Mpira wa Miguu ya Lipuli.
Mwenyekiti huyo amesema hayo jana mara baada ya kukabidhi kiasi cha Sh 4.5 Milioni kwa uongozi wa timu ya Lipuli kwa ajili ya safari ya kwenda Dar es Salaam kwenye mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya nane bora.
Tiimu hiyo imeondoka leo Ijumaa, Aprili 21, 2023.
Comred Yassin amesema kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Halima Dendego inaendelea na jukumu la kuwaomba wadau na wananchi kwa ujumla kuichangia timu ya Lipuli.
Amewashukuru wadau mbalimbali waliotoa michango yao na wale ambao wanatarajia kuichangia timu hiyo ya Lipuli.
"Michezo ina faida nyingi,
michezo ni fursa ya ajira kwa vijana wetu. Lakini pia michezo ni sehemu ya uchumi na inatuunganisha watu wote. Hivyo ni muhimu kwa wananchi wote kusapoti masuala ya michezo," amesema Yassin.
Aidha amemshukuru Mh Dendego kwa kuunga mkono kwa dhati suala la michezo Mkoani Iringa
Post A Comment: