Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Comred Daud Yassinamewakabidhiviongozi wa Chama cha Riadha cha watu wenye ulemavu Mkoani Iringa kiasi cha shilingi 850, 000/=
Comred Yassin ametoa fedha hiyo ili kufanikisha safari yao ya kwenda Dar es Salaam kwenye mashindano ya watu wenye ulemavu.
Kiongozi huyo wa CCM Mkoa wa Iringa amekabidhi kiasi hicho kutokana na maombi aliyopokea kutoka kwa viongozi wa chama hicho.
"Nafurahi kwamba mliniandikia kuniomba mchango wa tshs 850,000/= zimepatikana zote kama mlivyoniomba, ombi langu kwenu mkazitumie kama ilivyokusudiwa na hapana shaka mtarudi na ushindi," amesema Mwenyekiti Yassin
kwa upande wao vongozi hao wa Chama Cha riadha cha watu wenye ulemavu mkoani Iringa, wamemshukuru Comred Yassin, kwa moyo wake wa upendo kwao.
Post A Comment: