Mwenyekiti chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Daud Yassin akikabidhi kiasi cha shilingi millioni mbili kwa ajili ya kuisaidia timu ya Mkwawa Queens ya mkoani Iringa


Na Fredy Mgunda, Iringa.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin akikabidhi kiasi Cha Tsh Milioni 2 Kwa uongozi wa Timu ya Mkwawa Queens inayocheza Ligi kuu ya Soka la wanawake Tanzania inayotarajia kusafiri jumapili kwenda Dar,Kucheza na Simba Queens kiasi Cha TshMilioni 3.4 zinahitajika ambazo zilikuwa zikihitajika Kwa ajili ya safari hiyo .


Akikabidhi msaada huo Leo Kwa uongozi wa timu hiyo ,Yassin alisema chama Cha Mapinduzi kinatambua mchango mkubwa wa Timu ya Mkwawa Queens na Timu nyingine Katika michezo na kuwa kutokana na changamoto ya timu hiyo .


Hivyo alisema Katika kuunga mkono jitihada za Timu hiyo na jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Katika kuendelea michezo nchini wao kama CCM mkoa wa Iringa wataendelea kuuunga mkono jitihada hizo ikiwa ni pamoja na kusaidia sekta ya michezo ndani ya mkoa wa Iringa.


Alisema jitihada za Mkwawa Queens wanaziona na kuwa ili Timu hiyo kutimiza vema majukumu yake ni vema wadau kuendelea kuunga mkono Timu zote ndani ya mkoa .


"Niwapongeze Sana Uongozi wa Mkwawa Queens Kwa kuendelea kuwakilisha mkoa Katika soka la wanawake na sisi kama chama tupo pamoja "


Aidha Yassin alimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego pamoja na Viongozi wengine wa mkoa huo Kwa kuendelea kusaidia Timu .


Afisa habari wa Mkwawa Queens Francis Godwin alipongeza mchango huo wa chama na kuwa huo ni mchango mkubwa Kwa Timu kupokea .


Alisema Kwa Sasa Timu hiyo inasafari ya kwenda Dar es salaam kucheza na Simba Queens siku ya Jumanne na kuwa timu itaondoka Iringa Jumapili safari ambayo itaigharimu Timu Tsh Milioni 3.4 baada ya hapo inajiandaa Kwa mchezo wake Dodoma na Mkoani Lindi ambako ili kufanikisha Mzunguko uliobaki zaidi ya Tsh Milioni 10 zinahitajika .


Hivyo aliwaomba wadau kuendelea kuisaidia Timu hiyo na kumpongeza jitihada za mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego na uongozi wa CCM mkoa chini ya Mwenyekiti Daud Yassin na wote ambao wameendelea kuichangia Timu hiyo .

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: