Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Anamringi Macha ameshiriki Mkutano Mkuu wa 16 wa Chama Tawala RPF Nchini Rwanda🇷🇼 akimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM.
Mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho ambae pia ni Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.
Pamoja na Chama Cha Mapinduzi Mkutano huo ulihudhiriwa na viongozi mbali mbali wa Vyama vingine kutoka baadhi ya Nchi Barani Afrika na nje ya Bara hili.
Katika Mkutano huo Ndg. Macha aliwasilisha salamu za CCM zilizobeba Ujumbe Mahususi wa kuutakia kheri na Mafanikio makubwa Mkutano huo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿 Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Salamu hizo zilisisitiza Umuhimu wa kuendeleza na kuudumisha Uhusiano mzuri uliopo kati ya CCM na RPF na Nchi ya Tanzania 🇹🇿 na Rwanda 🇷🇼
Pamoja na Mambo mengine, Wajumbe walipokea na kujadili taarifa ya kazi za Chama cha RPF na Utekelezaji wa Shughuli za miradi mbali mbali ya Maendeleo na kufanya uchaguzi wa viongozi wa ngazi za kitaifa ikiwepo nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na katibu Mkuu wa RPF ambapo Mhe Paul Kagame alichaguliwa tena kwa Kura za kishindo kwa kupata 99.8% ya kura halali zilizopigwa.
Kwa nafasi ya Makamu mwenyekiti Chama hicho kiliweka historia kwa kumchagua Makamu mwenyekiti wa RPF ambae ni Mwanamke kwa mara ya kwanza Tangu kuanziashwa kwa Chama hicho.
Post A Comment: