KIGOMA
AFISA Madini Mkazi Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Pius lobe amesema kuwa uzalishaji wa chumvi katika mkoa wa Kigoma umefungua fursa mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa miradi ya kijaamii na ajira kwa wanawake.
Mhandisi lobe aliyasema hayo tarehe 8 Aprili, 2023 kwenye mahojiano maalumu ya kuelimisha umma kuhusu sekta ya madini yaliyofanyika katika mgodi wa Nyanza Mines Ltd wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Akieleza fursa zilizopo katika sekta ya madini katika mkoa wa kigoma yalichongiwa na uzalishaji wa chumvi, Mhandisi Lobe amesema kuwa kuwepo kwa mgodi huo umeweza kuajiri wanawake wengi zaidi ambao wanafanya shughuli za kuvuna na kupaki chumvi kwenye vifungashio maalum.
“Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha tunaongeza makusanyo ya serikali ili kufikia malengo ambayo tumewekewa na Tume ya Madini hadi sasa tumekusanya zaidi ya shilingi bilioni moja kuanzia Julai 2022 hadi sasa ambayo ni sawa na asilimia 87 ya lengo,”alisema Mhandisi Lobe.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Mgodi wa Nyanza Mines Limited Bonny Mwaipopo amesema kuwa uwepo wa kiwanda hicho imekuwa ni fursa kwa wakazi wa Uvinza, ambapo wakati wa uzalishaji wa chumvi wanaajiri takriban watu 1000 wanaofanya shughuli ya kuvuna na kupakia kwenye magari na kupeleka kwenye kiwanda cha kusafisha chumvi.
Aliendelea kusema kuwa uwezo wa uzalishaji wa mgodi kwa mwaka ni tani 45,000 ambapo kwa mwaka 2023 wamejipangia kuvuna tani 60,000 na kuuza ndani na nje ya nchi kama Burundi na Congo.
Naye Mkazi wa Uvinza, Salome Amos alishukuru serikali kupitia Tume ya Madini kwa kuhakikisha sheria zilizowekwa zinatekelezwa ambapo zimesaidia kuwapatia kivuko kinachowavusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kufuata huduma za afya na kijamii.
“Mwanzoni tulikuwa tunapata shida ya kuzunguka umbali mrefu lakini tunashukuru mgodi kivuko hiki kinatusaidia mtu akiugua anavushwa haraka na kwenda kupatiwa huduma.
Post A Comment: