Na Mwandishi wetu Kiteto

Kiteto. Ziara za Mawaziri wawili waliofika nyakati tofauti Kiteto, zimeanza kurejesha imani ya wananchi kwa Serikali yao kufuatia baadhi ya changamoto zinazowakabili kutatuliwa  zikiwemo migogoro ya ardhi.

Mawaziri waliofika Kiteto ni Dr. Abdallah Ulega aliyekiwa Naibu Waziri wa Mifugo na sasa na Waziri kamili (MB) na Feb 18.2023 Naibu waziri wa mifugo na Dr Festo Dugange (MB) Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi naye aliyefika Kiteto Feb 21.2023.

Dkt. Ulega akiwa Kiteto Feb 18.2023 alikuja kufufua ndoto za Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kuchimba bwawa kata ya Ndedo mwaka 1975 na kupasua 1978 ambapo aliahidi kuwa Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassani imetenga mil 500 kufufua ndoto hiyo

Feb 21.2023 Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Festo Dugange naye alifika Kiteto kukagua hospitali ya wilaya, namna huduma za afya zinavyotolewa ambapo alilalamikiwa na wazee wa Kibaya kisha kuagiza kufunguliwe dirisha la wazee huku akisema kiasi cha mil 900 kimetengwa na Serikali kukarabati hospitali hiyo.

 Baadhi ya wananchi akiwemo Maulidi Kijongo amesema kwa muda mrefu wamekuwa na changamoto nyingi na ambazo hazipata majibu  na ambazo kiongozi wa ngazi ya juu akifika ataona na kutatua.

"Kiteto tuna viongozi wanaotuongoza na tumekuwa tukishirikiana nao na kuwaeleza changamoto zetu ambazo mpaka sasa hazijatatuliwa sasa wanapofika viongozi wa ngazi ya juu hapa tukiwaeleza inakuwa rahisi hata kupata maelelezo toka juu na huenda wakatatua" alisema Kijongo

Kwa upande wake Waziri Yusuph (mwananchi wa Kibaya) alisema ana tatizo la mgogoro wa ardhi muda mrefu zaidi ya miaka saba haujatatuliwa na  amefika ngazo ya kijiji hadi wilaya hajapata ufumbuzi akisema ujio wa viongozi wa ngazi ya Taifa unaleta faraja kwao pale wanapokutana nao na kuwaeleza changamoto hizo

Akiwa Kiteto Dkt. Abdallah Ulega alizuia msafara wake na wananchi wa eneo la mlima wa simu wakiwa wamebebelea matawi ya majani wengine wakilia machizi wakimwomba awasikilize kilio chao ambacho kimedumu muda mrefu

"Tuna matatizo tuna matatizo tunaomba ututatulie Waziri...tuna mgogoro na Wakala wa msitu Tanzania TFS ambaye ametukuta kwenye maeneo yetu tukiyatumia kujipatia kipato, TFS Kiteto wamekuja na wazo la kihifadhi eneo hili, wakadai kutupa maeneo badala bika mafanikio tunakamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani kila mara kuwa tumevamia eneo hilo wakati TFS wametukuta hapo"alisema Ibrahimu Ally

Kufuatia kilio hicho Naibu waziri Ulega alilazimika kumpigia simu Meneja wa TFS Taifa Pro Santos Silayo kumweleza kilio hicho na kuahidiwa mbele ya wananchi hao kushughulikiwa tatizo hilo mara moja

"Wananchi wamenizuia gari langu wakiomba kutatuliwa mgogoro kati yao na TFS kuwa wananyanyaswa kwa kupigwa faini kwenye eneo lao linalodaiwa na TFS  kuwa ni hifadhi huku wao wakidai kuwa kuna makubaliano ambayo hayajafikiwa ya kupewa findia ili waondoke..mimi nakuelewa sana utendaji wako Pro naomba ushughulikie suala" alisema Ulega 

Akiwa Kata ya Ndedo Ulega aliwahakikishia wananchi waliokuwa na changamoto ya maji ya muda mrefu toka mwaka 1978 kuwa watakarabatiwa bwawa ambalo lilijengwa na Serikali ya awamu ya kwanza ambalo litagharimu zaidi ya mil 500

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Festo Dugange siku mbili baada ya Naibu Waziri wa mifugo Abdallah Ulega kuondoka naye alifika kukagua miradi ya maendeleo Afya na elimu na kuwaambia wananchi kuwa Serikali imejipanga kuwahudumia  kikamilifu

"Serikali imetoa mil 900 za ukarabati wa hospitali ya wilaya iwe na hadhi wananchi mpate huduma ya afya kikamilifu tofauti na awali mlilazimika kwenda Dodoma kufuata tiba wakati mngepatia hapa" alisema Naibu Waziri Dugange

Akizungumza na mzee Mtugutu Mwinyikai aliyefika hospitalini hapo aliyemweleza Naibu Waziri kuwa Hospitaki haina dirisha la wazee ambapo Dr Dugange aliagiza dirisha hilo lifunguliwe mara moja na wazee hao waanze kupata huduma hiyo kwa kuwa Sera ya CCM inaelekeza hivyo.

Katibu wa CCM Kiteto Denis Mwita alipongeza ziara za mawaziri hao Kiteto akisema zimeleta mwanga kwa wananchi kuwa na imani zaidi na Serikali yao baada ya kutopata utatuzo wa changamoto zao muda mrefu

"Ni kweli viongozi wa ngazi ya juu wakifika eneo husika mara kwa mada kuna mabadiliko...na hata hivi tunajiandaa tena kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo pamoja na mambo mengine yeye atakuja kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM" alisema Mwita Katibu wa CCM Kiteto.


Share To:

Post A Comment: