Na John Walter-BabatiWatumishi wanawake wa Mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Manyara (TRA) imetoa msaada kwa watoto yatima na waishio katika mazingira magumu katika kituo cha Manyara Holistic Centre (MAHOCE).
Msaada uliotolewa na wanawake hao ni mchele kilo 75, maharage 25, ngano kilo 150, mafuta ya kupikia lita 30, sabuni ya unga mifuko mitatu, sukari kilo 50, madaftari na sabuni ya mche boksi tatu.
Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi (TRA) mkoa wa Manyara Serapio Luanda aliyeongozana na Wanawake hao, amesema wameamua kuwatembelea watoto hao kuwatia moyo kusoma kwa bidii ili watimize ndoto zao.
Mwakilishi wa Kituo cha MAHOCE, Anderson Mbwambo amesema misaada hiyo inawafariji watoto hao na kujihisi furaha huku akishukuru kwa upendo waliounesha TRA.
Watumishi wanawake wa mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Manyara wanaadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo kilele chake ni jumatatu Machi 13, 2023.
Wanawake katika mji wa Babati wameamua kuungana kwa pamoja kusheherekea siku ya wanawake Duniani kwa kufanya mazoezi ya mwili na kutoa misaada mbalimbali kwa makundi mbalimbali katika jamii.
Post A Comment: