Wito huo umetolewa mapema leo na Meneja wa wakala wa Vipimo Mkoa wa Geita , Balisco Kapesa wakati akiongea na mawakala pamoja na wafanyabiashara Mkoani humo.
Amesema bado wapo baadhi ya wafanyabiashara wanaouza mitungi ya gesi bila kupima kitu ambacho ni kinyume na sheria kwani uzito unatakiwa kuonekana kabla ya mtumiaji wa mwisho hajaanza kutumia.
“Ni kosa kisheria kuuza gesi bila kuwa na mizani kwahiyo mnapaswa kuhakikisha mnakuwa na mizani ili kuepuka hatua Kali za kisheria kwa wale watakaobainika niombe ifikapo Aprili 1,2023 wote muwe na mizani”Balisco Kapesa Meneja wa wakala wa Vipimo Mkoa wa Geita.
Kapesa ameongezea kuwa ni vyema kwa mtumiaji wa gesi akaona na kuhakikisha muuzaji akiwa amepima na amejiridhisha kabisa kuwa ni kiwango stahiki na kama ni pungufu anaona.
Post A Comment: