Naibu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taaluma (DIT), Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof.Ezekiel Masige Amri akifungua Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Kituo cha Umahili wa Tehama DIT, Dkt.Petro Pesha akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam. Bw.Alexius Revocatus Kagunze kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bw.Abraham Mangesho akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam. Badhi ya wanafunzi wa Kidato cha tatu Shule za Sekondari nchini wakiwa katika ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Tano ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike, Mafunzo ambayo yanafanyika katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Jijini Dar es Salaam.
**********************
NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imefungua Mafunzo ya Siku Tano (5) ya TEHAMA kwa wanafunzi 96 wa kike wa kidato cha tatu shule za Sekondari nchini ambapo yanafanyika katika Ukumbi wa DIT kuanzia leo Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) yamefunguliwa na Naibu Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Taaluma (DIT), Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof.Ezekiel Masige Amri kwa niaba ya Mkuu wa Taasisi hiyo.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo hayo leo Machi 13,2023, Prof.Amri amepongeza juhudi kubwa iliyofanyika katika kuhakikisha mafunzo yanatolewa kwa mabinti wa shule za sekondari yatakwenda vizuri na kupata mrejesho mzuri kutoka kwa wahusika wa mafunzo hayo.
Prof.Amri ameushukuru mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuona umuhimu wa TEHAMA kwa vijana hasa jinsia ya kike kwa kuwa vijana wa kike siyo wengi kwani wanaogopa masomo ya sayansi hivyo mafunzo haya yatakuwa chachu ambayo itasaidia kuleta uwiano sawa na ule wa vijana wa kiume.
Aidha amewaeleza wanafunzi umuhimu wa TEHAMA kwa kipindi hiki ya kwamba "Katika dunia ya sasa hakuna jambo linaloleta mapinduzi ya haraka kama TEHAMA na sasa hivi tupo kwenye Mapinduzi ya nne ya viwanda hii inapelekea mahitaji makubwa ya Teknolojia".
.." niwaambie tu kuwa mawasiliano mengi sasa hivi yanatumia Tehama, kadhalika viwanda vinahitaji mifumo inayojiendesha yenyewe ikisaidiwa na Tehama kwa hiyo wataalam katika sekta hii wanahitajika hivyo hii ni fursa ya pekee kwenu" amesema Prof.Amri
Sambamba na hilo Prof. Amri ameeleza kuwa nchi yetu inatambua umuhimu wa kuandaa wataalam wa Tehama katika nyanja mbalimbali na ndiyo sababu kubwa ya Ofisi ya Rais TAMISEM kwa kushirikiana na UCSAF wameweza kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) katika kuhakikisha wanawapatieni ninyi mafunzo yatakayowasaidia ili muwe chachu kwa vijana wengine wa kike.
Kwa upande wake Bw.Alexius Revocatus Kagunze kutoka Ofisi ya Rais TAMISEM amewasisitiza wanafunzi kutumia fursa hii vizuri kwani dunia ya sasa bila Tehama itakuwa vigumu kushindana ndani na nje ya nchi.
Alexius amesema "Niwaombe vijana wote mliopata nafasi ya kufika DIT kwa ajili ya mafunzo kuwa makini katika kusikiliza na kuuliza maswali, niwaambie tu kuwa dunia ya sasa ni ya Teknolojia na hiyo ndio itakayotusaidia ili tuweze kushindana kimataifa na dunia nzima na bila hiyo sisi kama nchi tutabaki nyuma na kutegemea wataalam kutoka nje ya nchi sisi kama Serikali tunaahidi kuwa tupo nyuma yenu kama walezi na wazazi kuhakikisha mnapata mafunzo yatakayowapatia ninyi utalaam".
Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Abraham Mangesho amesema kuwa mfuko unajitahidi kufadhili mafunzo haya ya Tehama ili kujenga uelewa kwa wasichana na kuwapa hamasa ili waone kuwa wao pia wanaweza kusoma masomo ya Sayansi au Tehama kwani jinsia hii inaonekana kubaki nyuma hivyo kupitia mafunzo haya ya siku tano tunaamini chachu itakayojengwa ndani yao italeta uthubutu wa kusoma Tehama ili waweze kuwa wataalam.
Post A Comment: