Na Denis Chambi, Tanga.
WAFANYABIASHARA wa vyakula katika masoko ya Mgandini na Ngamiani yaliyopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Tanga wamelia na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo miundombinu mibovu iliyopo licha ya ushuru wanaotozwa hali ambayo inachangia kuharibika kwa bidhaa zao kabla ya kuuza.
Wakizungumza mbele
ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Rajab Abdurlahman
March 29,2023 katika ziara yake ya kutembelea, kujua upatikanaji wa bidhaa na hali
ya bei ilivyo hususani kipindi hiki katika masoko hayo walisema kuwa
pamoja na bidhaa kupatikana na wastani na bei kuwa ya kawaida bado
uchakavu wa miundo mbinu imekuwa ni tatizo sugu kwao licha ya viongozi
na serikali kutoa ahadi za mara kwa mara kuwawekea mazingira rafiki.
Katibu
wa soko la Mgandini Shabani Mohammedi alisema kuwa licha ya
wafanyabiashara waliopo katika soko hilo kuchangia shilingi elfu tisa
kila mwezi kulingana na maelekezo ya halmashauri ya jiji la Tanga lakini
bado hawaoni faida yake kutokana na kuendelea kufanya baishara zao
katika mazingira magumu hasa kayika nyakati za mvua.
"Tuna
kilio cha muda mrefu cha kujengewa soko tunalipa ushuru kama kawaida na
hakuna mfanyabiashara aliyekataa n tumekuwa tukiahidiwa muda mrefu
kujengewa soko lakini halijengwi , ukiachana na hilo kuna malori
yanayoingia hapa ni mengi ambayo yanaweza kusaidia kuwezesha kuchangia
mapato kwa kulipia ushuru " alisema Mohammed.
Mmoja
wa wafanyabiashara wanaouza viazi katika soko la Mgandini alisema kuwa
bidhaa hiyo ambayo wamekuwa wakiipata nje ya mmoa wa Tanga wamekuwa
wakikutana na changamoto ya usafiri wakitozwa ushuru kuwa mkubwa kila
mahali wanapopita kabla ya kufika sokoni hapo wakiwa na hayimaye
kuambulia tu hasara.
"Wateja
kipindi hiki cha Ramadhani sio wengi kivile tunakutana na changamoto
njiani wakati tunasafirisha mzigo kutoka shambani hasa sisi wa viazi
serikali ijue kwamba sisi hatupati faida tunapata hasara tunatozwa
ushuru mkubwa njiani na tukifika hapa sokoni viazi vinaoza"
Akizungumza
mara baada ya kujionea hali ya upatikanaji wa bidhaa, bei na
miundombinu ilivyo katika masoko yote mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi 'CCM' Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman alisema kuwa
wamejipanga kufanya ziara katika masoko yote yaliyopo mkoani humo kwa
lengo la kujua changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara na kuona
namna nzuri ya kuweza kuzitatua kwa manufaa ya wananchi wote.
"
Ziara yetu ya leo tumekuja kuangalia hali ya upatikanaji wa bidhaa
pamoja na hali ya bei zake lakini nitarudi sasa maalum baada ya mwezi
mtukufu wa Ramadhani kufanya ziara mkoa mzima wa Tanga na ikiwemo
katika mji wa Tanga wenyewe na katika soko hili la Mgandini ndio hasa
pana changamoto kubwa soko hili mmeahidiwa kwa muda mrefu na
halijengwi miundombinu yake ya hovyo hivyo lazima miundombinu ikae
katika hali nzuri ili mraji wa mwisho aweze kufaidika apate matunda ya
nchi yake" alisema Rajab.
"Nitafanya
ziara mahususi katika mkoa mzima wa Tanga kila halmashauri watueleze
wamejipangaje kuondoa kilio cha muda mrefu cha wafanyabiashara
kuwaboreshea miundo mbinu katika mazingira yaliyo mazuri maana mwisho wa
siku ukimboreshea mfanyabiashara unafanya afya ya mlaji nayo iweze
kuimarika lakini sio katika hali iliyopo sasa haitulidhishi tunaamini
serikali itafanyia kazi ushauri ambao tunatoa" aliongeza.
Hata
hivyo licha ya kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
ambapo awali ilizoeleka kuwa bei za bidhaa na vyakula vingi kupanda
lakini katika masoko hayo bei ipo kawaida kama siku zote huku bidhaa
zikitajwa kuadimika kutokana na kipindi cha ukame wa baadhi ya maeneo
hii ikichangiwa na ukosefu wa mvua za kutosha.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi 'CCM' Mkoa wa Tanga
Rajab Abdulrahman akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa Nyama
waliopo katika soko la Ngamiani jijini Tanga wakati alipofanya ziara
yake ya kutembelea masoko kujua hali ya upatikanaji wa bidhaa na bei
zake katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
jumatano.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi
'CCM' Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahman akizungumza na mmoja wa
wafanyabiashara wa vyakula waliopo katika soko la Mgandini lililopo
jijini Tanga wakati alipofanya ziara yake ya kutembelea masoko kujua
hali ya upatikanaji wa bidhaa na bei zake katika kipindi hiki cha
mfungo wa mwezi mtukufu aa Ramadhani juzi jumatano.Picha na Denis Chambi
Tanga.
Post A Comment: