Julieth Ngarabali ,Kibaha
Wadau wa elimu wameiomba Serikali kuongeza ajira za walimu wa Elimu maalumu nchini ili kuwezesha watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali kupata fursa ya kijifunza kuanzia elimu ya awali,msingi na kuendelea kwa ukamilifu kama ilivyo kwa wengine wasio na changamoto hiyo.
Ombi hilo limetolewa na wadau hao huko Mjini Kibaha Mkoani Pwani waliohudhuria kikao cha wakuu wa shule, maafisa Elimu Msingi na sekondari kutoka Halmashauri zote Mkoani humo chenye lengo la kufanya tathmini ya maendeleo ya Elimu kwa miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
"Hili kundi nalo ni muhimu kupata elimu lakini changamoto uhaba wa walim mfano tu s isi Halmashauri ya Bagamoyo tuna upungufu wa walimu 12 wa elimu maalumu maana waliopo ni 17 tu, "amesema Wema Kajigili.
Kajigili ambaye ni Afisa Elimu awali na Msingi Wilayani Bagamoyo amesema changamoto hiyo ni vema ikafanyiwa kazi kwa wakati kwani walimu hao wanaumuhimu hasa kukuza uelewa kwa wanafunzi wenye ulemavu ikiwemo uziwi katika kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK)
Naye Afisa Elimu taaluma Halmashauri ya Chalinze Hamisi Shemahonge amesema uuwiano wa walimu wa Elimu maalumu hauendani na mahitaji jambo ambalo linawapa ugumu wanafunzi wenye uelemavu wakati wa kijifunza.
Awali akifungua kikao hicho , Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Severa Salvatory aliwataka wadau hao kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kujiwekea malengo ikiwemo kupambana na changamoto zilizopo kwani lengo ni kuhakikisha kundi hilo nalo linapata elimu.
"Fanyeni vikao mara kwa mara kulingana na miongozo iliyopo Ili kupata tathmini na mwenendo wa kazi na kama kuna changamoto mnazifanyia kazi kwa wakati"amesema.
Aidha Afisa Elimu Mkoa wa Pwani Sara Mlaki amewaelekeza Maafisa hao pamoja na wakuu wa Shule kuhakikisha wanaifanyia kazi changamoto ya kuondoa tatizo la baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika maarufu (KKK) Ili kukuza kiwango cha elimu.
Mlaki amesema taarifa alizopata ni kwamba hali hiyo inachangia na wanafunzi wanaohamia kutoka mikoa mingine wanakuwa na tatizo hilo hivyo ni vema wakabainishwa Ili kupata ufumbuzi wa kukabiliana nalo.
Sekta ya elimu na mafunzo kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa maendeleo ya Taifa
Sekta ya elimu na mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo
ya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleo
ya Taifa 2011/12 hadi 2024/25, inatarajiwa kuleta maendeleo
ya haraka ya rasilimaliwatu kwa kutayarisha idadi ya kutosha
ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili
kulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa kati na shindani ifikapo mwaka 2025.
Mwisho
Post A Comment: