Na Denis Chambi, Tanga.
Halmshauri ya jiji la Tanga imetenga
eneo lenye ukubwa hekari mia mbili kwaajili ya kilimo ambalo
wanatarajia kuligawa kwa vijana wapatao 200 ili waweze kujishughulisha
na Kilimo kwa lengo la kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.
Akitoa
taarifa hiyo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dkt. Sipora Liana amesema
kuwa eneo hilo ambalo lipo Mleni kata ya Mabokweni bado ni pori
wanatarajia kulisafisha kwa kushirikiana na shirika la Botner Foundation
tayari kwa ajili ya kuligawa kwa vijana hao.
Alisema
kutokana na jiograhia ya Tanga aridhi yake ambayo inastawi mazao
mbalimbali itasaidia sana kuufungua mkoa huo kupitia sekta ya kilimo
hii ikienda kuakisi kwa vitendo kauli mbiu ya sasa inayosema 'Tanga
lango kuu la uchumi Afrika Mashariki'.
"Tumeweza
kupate eneo la hekari mia mbili tutalisafisha tukishirikiana na
shirika la Botner foundation tuweze kuwagawia vijana zaidi ya mia nane
waweze kulima, tunajua sisi Tanga tuko kwenye lango la uchumi wa Afrika
Mashariki tukipanda mazao yeyote yale ni rahisi sana kusafirishwa,
mheshimiwa Rais katuboreshea bandari yetu ya Tanga ambayo itakuwa ni
rahisi sasa kupeleka mazao yetu visiwa vya Comoro, Pemba au Unguja
mazao yeyote tunajua watu wa maeneo haya wanakuja kuchukua mboga mboga
hapa Tanga" alisema Dkt Liana.
Alisema
katika kuimarisha zaidi sekta ya kilimo katika eneo hilo halmashauri
hiyo imejipanga kuweka miundo mbinu ya umwagiliaji hatua ambayo
itawasaidia vijana hao kwa asilimia kubwa na hivyo kuweza kuchangia
pato la Taifa na kujipatia kipato.
"Sisi
jiji la Tanga tumedharia katika hilo eneo la hekari mia mbili tutaweka
miundombinu kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji kwahiyo vijana wetu
watagaiwa na tunaamini kwamba wimbi la vijana ambao hawana watapata
shughuli za kufanya, tunaamini mpaka ikifika 2025 tutakuwa sehemu
nzuri" aliongeza.
Aidha alimpongeza na kumshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo
halmashauri hiyo ilipokea shilingi Million 540 kwaajili ya ujenzi wa
soko jipya la wamachinga katika Soko la Mlango wa Chuma ambalo bado
ujenzi wake unaendelea hadi sasa.
"
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa mwaka jana 2022
alileta fedha Million 540 kwaajili ya kujenga soko jipya la wamachinga
lile soko tunaendelea nalo pale na tumefika hatua nzuri sasa hivi sisi
Halmashauri tumeongeza mapato ya ndani shilingi 360 ili kuweza
kuendeleza pale ambapo soko limeishia kwa sababu soko lenyewe ni kubwa
na wamachinga waliopo ni wengi" aliongeza Dkt. Liana.
Sambamba
na hayo halmashauri ya jiji la Tanga ilipokea kiasi cha shilingi 470
kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Magaoni
wakimshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua hiyo
ikiwa ni miaka miwili imetimia katika awamu ya sita ya utawala wake.
"Lakini
pia Mheshimiwa Rais ameleta Million 470 kwaajili ya ujenzi wa shule
mpya ya Magaoni ile shule ina kila kitu imejengwa maabara maktaba na
miundombinu mingine lakini ameleta pia milion 450 kwaajili ya ukarabati
wa shule ya sekondari ya Usagara na Million 500 kwaajili ya ujenzi wa
kituo cha afya Tongoni" aliongeza.
Dkt
Liana aliongeza kuwa wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo agizo la
serikali katika usimamizi wa ukusanyaji mapato ya ndani ambapo kwa
kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 jiji la Tanga lilivuka lengo kwa
kuweza kukusanya Billion 17 ambapo lengo walilopangiwa lilikuwa ni
Billion 15 na mwaka huu wakipangiwa kukusanya Billion 18 mpaka December
2022 wakiwa tayari wamefikia asilimia 50.
Post A Comment: