Na John Walter- Manyara

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dr. Dorothy Gwajima amesema vazi rasmi litakalovaliwa  katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2023 ni batiki.

Gwajima ameyasema hayo leo Machi 1, 2023 akiwa Babati mkoani Manyara kuelekea Arusha ambapo amesema lengo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi na ubunifu wazalishaji wa ndani hususani wanawake.

DR.Gwajima amesema kwa kuwa wanawake wajasiriamali ni kundi muhimu katika kukuza uchumi wa pato la taifa, ameelekeza mikoa na wadau wote kwamba katika kuwaunga mkono, vazi la batiki litumike kama sare rasmi katika maadhimisho ya mwaka huu.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2023, " Ubunifu na mabadiliko ya Teknolojia, chachu katika kuleta usawa wa kijinsia"

Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka kuanzia Machi 1 na kufikia kilele Machi 8 ambaapo kwa mwaka huu yanafanyika kila mkoa yakiratibiwa kupitia ofisi ya wakuu wa mikoa na halmashauri zote nchini.

Share To:

Post A Comment: