*********************
UNESCO kupitia mradi wake wa O3 na O3 Plus kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yawanoa walimu watarajiwa waliopo Kwenye chuo kishiriki cha elimu Dar es salaam (DUCE) juu ya ufundishaji wa stadi za maisha, VVU, Afya ya Uzazi, ukatili wa kijinsia na kuhusiana Kwa heshima.
Wanafunzi 200 waliopo Kwenye masomo ya ualimu DUCE, wamepata fursa ya kufundishwa jinsi ya kutumia mfumo wa tehama wa Taasisi ya Elimu Tanzania wenye miongozo ya jinsi ya kufundisha wanafunzi kuhusu masuala ya stadi za maisha, VVU, Afya ya Uzazi, ukatili wa kijinsia na kuhusiana Kwa heshima Kwa kuzingatia umri na maadili.
UNESCO Kwa kupitia mradi wa O3 Plus inafanya kazi na vyuo vikuu na Vyuo Vya kati 16 Tanzania bara na Visiwani.
UNESCO inaunga mkono na kusaidia juhudi za serikali ili kuhakikisha elimu ya kina ya stadi za maisha inayozingatia afya ya uzazi, VVU/UKIMWI na unyanyasaji wa kijinsia inawafikia vijana wote kwa kuzingatia umri, maadili na tamaduni za kitanzania.. Kwa kusaidiana na TET UNESCO imesaidia kuweka miongozo ya kufundishia mada hizo mtandaoni.
Post A Comment: