Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa habari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juu ya namna ya kuwasilisha habari kwa jamii zitakazozingatia Usawa wa Kijinsia yaliyofanyika leo Machi 20,2023 Jijini Dar es Salaam Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka TGNP, Bi. Monica John akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa habari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juu ya namna ya kuwasilisha habari kwa jamii zitakazozingatia Usawa wa Kijinsia yaliyofanyika leo Machi 20,2023 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara Uandishi wa habari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (SJMC) Dkt. Dotto Kuhenga akizungumza wakati wa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa habari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juu ya namna ya kuwasilisha habari kwa jamii zitakazozingatia Usawa wa Kijinsia yaliyofanyika leo Machi 20,2023 Jijini Dar es Salaam

Wanafunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa habari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (SJMC) wakiwa kwenye mafunzo yanayotolewa na Mtandao wa Kijinsia (TGNP) juu ya namna ya kuwasilisha habari kwa jamii zitakazozingatia Usawa wa Kijinsia yaliyofanyika leo Machi 20,2023 Jijini Dar es Salaam

Wawezeshaji wa Mafunzo kutoka TGNP wakipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa habari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (SJMC) baada ya Mafunzo juu ya namna ya kuwasilisha habari kwa jamii zitakazozingatia Usawa wa Kijinsia yaliyofanyika leo Machi 20,2023 Jijini Dar es Salaam.

****************************

NAEMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imetoa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Shule Kuu ya Uandishi wa habari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (SJMC) juu ya namna ya kuwasilisha habari kwa jamii zitakazozingatia Usawa wa Kijinsia na kujenga Viongozi watakaoleta Usawa.

Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka TGNP, Bi. Monica John amesema mafunzo hayo yametokana na Mradi wa Boresha habari wenye lengo la kuwawezesha wanahabari chipukizi kuandika na kutoa taarifa ambazo zitaepuka ukandamizaji wa kijinsia bali kuleta usawa na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi.

"Niendelee kuwapa hamasa waandishi wa habari wanawake pamoja na wanaume kuona ni kwa namna gani wakiwa wanaripoti zao kuangalia je, taarifa hizo zimeweza kubeba mlengwa wa kijinsia kwa maana watoa taarifa tunaowatumia kwenye taarifa zetu za habari kwa kuweza kuweka usawa kwa wanaume na wanawake". Amesema

Amesema kwenye suala la jinsia tunaangalia rasilimali pamoja na fursa zote ambazo zinapatikana ziweze kunufaisha makundi mbalimbali ambayo yapo kwenye jamii hasa yale ambayo kwa kiwango kikubwa yameweza kuachwa nyuma.

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba amesema wameweza kuwafikia waandishi wa habari waliopo shuleni kwani wakiweza kuelewa masuala ya jinsia katika kuripoti habari wataweza kuchochea maendeleo katika Taifa letu kwasababu jamii itapata elimu na kuzingatia usawa wa kijinsia.

"Tunaamini suala la gender ni suala mtambuka ambalo linaweza likaingizwa katika kila eneo, tunaliingia kwenye afya, kwenye elimu, kwenye kilimo na maeneo mengine mengi ili kuleta usawa wa kijinsia ". Amesema

Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki Mafunzo hayo wameipongeza TGNP kwa kwaandalia mafunzo hayo kwani yatawasaidia kuondokana na ubaguzi kwenye utoaji wa taarifa zao ikiwemo kushirikisha jinsia zote kwenye habari watakazofanya
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: