Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Christopher Myava akitoa taarifa ya ufuatiliaji katika kipindi cha robo ya Oktoba hadi Desemba 2022 kwa waandishi wa habari Mjini Kibaha ambapo kipindi hicho wameweza kubaini udanganyifu kwenye miradi 75 ya Maendeleo yenye thamani ya sh. Bil. 11.4. Picha Juliet Ngarabali
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Mkoani Pwani imefanya kazi ya ufuatiajii katika miradi 75 ya Maendeleo yenye thamani ya sh. 11,421,038,710 katika sekta za elimu,afya ,maji na barabara na kubaini mapungufu mbalimbali ikiwemo kutumia vifaa vilivyp chini ya viwango
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha wakati akitoa taarifa ya kipindi cha robo Oktoba hadi Desemba 2022, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Christopher Myava alisema kuwa mapungufu hayo yamebaibika baada ya kufanyika uchunguzi
Myava amesema moja ya miradi hiyo ni mradi wa Shule mpya ya Sekondari ya Viziwaziwa iliyopo Mjini yenye thamani ya sh. 470 ,000,000 ambapo mabati ya yaliyotumika kuezekea jengo la utawala ,maabara na vyoo vya shule hayakuwa ya kiwango kwani walitumia ya geji 30 badala ya geji 28 kama Serikali ilivoelekeza.
Mradi mwingine ni wa ukarabati skimu ya maji Kijiji Cha Mkongo (Rufiji) yenye thamani ya sh. 512, 208,446 Milioni ambapo imebainika katika tanki moja la kuhifadhia maji linavujisha na milango ya jengo la Ofisi ya Jumuia ya watumiaji maji Kijijini humo haikuwekwa kwa ubora.
Aidha katika eneo la uchambuzi wa mifumo tayari chambuzi za mfumo imefanyika ili kuweza kudhibiti mianya ya rushwa katika Idara za Serikali na sekta binafsi chambuzi na mifumo mitatu zilifanyika .
kwenye maeneo ya uendeshaji na usimamizi wa masoko ya biashara na utekelezaji masoko ya biashara pamoja na
Utekelezaji miradi kwa kutumia force akaunti katika vyama vya ushirika vya mazao na masoko (AMCOS ) vya Mkongo,Kilimani, ,kitupa ,nyaminywili ,kipo na ngorongo ( AMCOS zote za Rufiji ).
," Katika uchambuzi huo yaliyobainika na hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuwepo udhaifu katika utunzaji wa nyaraka na kumbukumbuku za vyama vya ushirika ambapo baadhi ya nyaraka zimekuwa zikitunzwa nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Bodi mfano KIPO MCOS Rfuji baadhi ya nyaraka za ushirika zilionekana kuharibiwa na mchwa." Amesema na kuongeza
" Hatua hii ya kukosa kumbukumbu ya nyaraka zilizoharibika inasababisha changamoto katika kubaini mapato na matumizi,takwimu na taarifa zote za fedha Kwa ujumla" amesema
Aidha katika eneo la uchunguzi, TAKUKURU imepokea malalamiko 87 kati yake 49 yalihusu rushwa na majalada mapya ya uchunguzi yamefunguliwa uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.
Kuhsu malalamiko 38 hayakuhusu Rushwa na kati yake 37 walalamikaji walishauriwa na lalamiko moja lilifunhiliwa.
"Mchanganuo wa malalamiko kisekta na idadi yake kwenye mabano ni Afya (4) , Ardhi (11) , bandari (1), baraza la ardhi ( 5) , elimu ( 4) , Mahakama ( 3) , mazingira (1) , Polisi (6) , TAMISEMI (35 ) , Ujenzi ( 1) , Ulinzi ( 3 ) ,ushirika (4), binafsi ( 1), mifugo ( 1 ) , fedha (1), miundombinu barabara ( 2) , maji ( 1) , maliasili ( 1) RITA ( 1) na Viwanda (1).
Mwisho
Post A Comment: