Na Nadhifa Omar, Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.George
Simbachawene amesema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kutoa
ushirikiano unaostahiki kwa kamati ya Afya na masuala ya UKIMWI kutekeleza
majukumu kwa kufuata miongozo,maoni na ushauri unaotolewa na kamati hiyo.
Kauli hiyo amaitoa leo Machi12 ,2023 baada ya Tume ya kudhibiti UKMWI
Tanzania (TACAIDS) kuwasilisha Taarifa kuhusu muundo na majukumu yake kwa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika Ukumbi wa Ofisi
za Bunge jijini Dodoma.
Awali akiwasilisha taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard
Maboko amesema TACAIDS ni Idara inayojitegemea chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na
imeanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.22 ya mwaka 2001 na Marekebisho yake Na.6
ya mwaka 2015, sheria hiyo ni kwa ajili ya Tanzania Bara pekee. Zanzibar ipo
Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).
Dkt. Maboko ameyataja majukumu ya TACAIDS kuwa ni kuandaa sera na miongozo
kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI nchini pamoja na kusimamia athari zake,
kusimamia mpango mkakati kwa ajili ya mipango ya programu za UKIMWI pamoja na
masuala mtambuka yahusuyo virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Kujenga mahusiano ya kitaifa na kimataifa kwa watu wote wenye UKIMWI kwa
kufanya uratibu wa masuala ya UKIMWI,kutafuta raslimali fedha ,kuzigawa na
kuzifuatilia katika programu za Mwitikio wa UKIMWI,kusambaza taarifa kuhusu
UKIMWI na madhara yake na programu za kuzuia na kudhibiti.
Kukuza tafiti ,upashanaji taarifa na kutunza kumbukumbu zinazohusiana na
udhibiti wa UKIMWI nchini,kukuza uraghibishi na utoaji wa elimu kwa ngazi ya
juu kuhusu kuzuia na kudhibiti UKIMWI, kufuatilia na kutathimini
shughuli zote za UKIMWI zinazotekelezwa nchini.
Aidha ameongeza kuwa shughuli nyingine ni Kuratibu shughuli zote za UKIMWI na kuzisimamia kwa mujibu wa mkakati wa Taifa wa UKIMWI, kwa kushirikiana na sekta
binafsi husika kuwezesha juhudi za upatikanaji wa tiba na kuhamasisha
upatikanaji wa tiba na matunzo na chanjo.
Jukumu lingine ni kuhamasisha haki na wajibu kwa watu wanaoishi na VVU
,kuhamasisha WAVIU kuishi kwa matumaini na kushauri serikali kuhusu masuala
yote yanayohusu kuzuia na kudhibiti UKIMWI ,kutambua vikwazo katika utekelezaji
wa kuzuia na kudhibiti katika sera na programu ,kusimamia shughuli zote
zinazohusiana na kuzuia na kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI,pamoja na
kushirikiana na sekta nyingine husika,kufanya shughuli nyingine za kuzuia na
kudhibiti VVU na UKIMWI.
Dkt. Maboko amesema utekelezaji wa majukumu ya TACAIDS unaongozwa na sera
,sheria ,kanuni ,mikakati na miongozo ikiwa ni pamoja na sheria ya tume ya
kudhibiti UKIMWI Tanzania Na,22 ya mwaka 2001na marekebisho yake Na6 ya mwaka
2015,Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001.
Mwongozo wa uraghibishi na mabadiliko ya tabia,Mwongozo wa VVu na
UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza,
mwongozo wa kusshughulikia makundi maalum kuhusu UKIMWI kwa kushirikiana na
Wizara ya Afya ,mwongozo wa jinsia na UKIMWI
,Mwongozo wa UKIMWI na haki za binadamu ,Mwongozo wa kufundishia kamati za
kudhibiti UKIMWI ngazi za Halmashauri,kata na vijiji, pamoja na mwongozo wa
kuunda kamati za kudhibiti UKIMWI kwenye mikoa,mwongozo wa kuunda kamati za
kudhibti UKIMWI kwenye Halmashauri.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Stanslaus Nyongo iliipongeza TACAIDS kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kudhibiti na kupunguza maambukizi ya VVU nchini na kuagiza kuendelea kufanyia kazi ushauri na maekezo yaliyotolewa na kamati hiyo,ikiwa ni pamoja na kufanya ufatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za chini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Afya na Masuala ya UKIMWI, Stanslaus Nyongo akizungumza na wajumbe pamoja na watendaji wa TACAIDS
na Ofisi ya Waziri Mkuu waliohdhuria kikao cha kamati hiyo walipokutana leo
jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene na Katibu Mkuu Dkt. Jimmy Yonaz (kulia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard Maboko alipokuwa anawasilisha Muundo na Majukumu kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Mhe. Seif Salum Seif akichangia wakati wa kikao cha kamati hiyo na TACAIDS kuhusu kubadilisha jumbe zinazotumika kwenye vibao vya ujenzi vinavyo tumia maneno ya Unyanyapaa.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI Mhe Hassan Mtega akichangia wakati wa kikao cha kamati hiyo umuhimu wa TACAIDS kufatilia utekelezaji wa majukumu ya kamati za UKIMWI za ngazi za chini.
Post A Comment: