Mkurugenzi wa Fundi smart Tanzania  Fredy Herbet akiongea na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa app ya fund smart 
Mamia ya mafundi smart waliojitokeza leo

Na Fredy Mgunda, Iringa.


MAFUNDI Mkoani Iringa wametakiwa kuunda vikundi ili waweze kupata  fursa mbalimbali za kiserikali zinatokea pamoja na kupata mikopo kwa urahisi.

Akizungumza wakati wa kongamano la Mafundi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego ambae ndiye alikuwa Mgeni Rasmi alisema kuwa kufungua app   hiyo ya mafundi smart kutapelekea kazi za mafundi kuonekana kwa urahisi  na kuwa kidigtari zaidi.

“Leo tumekutana hapa ili kuzindua app ya fundi smart tunatambua  nchi yetu na dunia nzima imewekza katika kidigitali katika ubunifu kwa matumizi  ya kitknolojia kwa sababu mageuzi haya ndiyo yatakayotuwezesha  kuwafikia wateja wetu kwa wakati muafaka watu tunaowahudumia kwa karibu na kuweza kutimiza ndoto ambazo sisi mafundi tumejiwekea kwa hiyo tumtumia hii teknolojia ya mawasiliano vizuri katika kipindi kizuri na muafaka muda muafaka kubwa ni kuwekeza muda juhudi akili na maarifa ili kutuwzsha kufika tunapopahitaji"

Aidha mkurugenzi wa Fundi smart Tanzania  Fredy Herbet alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha mafundi wa aina tofauti tofauti huku akiwaasa mafundi kuwa waaminifu kwa wateja wao pindi wanapopata kazi.

“Matamanio yetu ni makubwa sana kwa sababu tayari tunamafundi 30000 tanzania wote tumeshawasajili cha kufanya ni kwamba matgemo yetu ni kuona kwamba fundi kwanza anahshimika anabadilisha mtazamo kutoka kuwa fundi wa kawaida anakuwa fundi smart ambaye halalamikiwi na wateja kwa sababu kumekuwa na mtazamo hasi kwa mafundi ndo maana wanasema fundi mkweli ni kinyozi kwa sababu hawa mafundi sio wakweli trust ni tatizo kubwa snaa kwa mafundi lakini eneo jingine hawa mafundi pia mambo mengi wamkuwa hawafanyi kinachotakiwa kuna baadhi ya mafundi wanaharibu vitu badala ya kutengeneza  kwa hiyo tunataka ufundi ulet matokeo chanya na ulete maendeleo kwa sababu wengi hawafurahii ufundi wao"

Kwa upande wao baadhi ya mafundi waliohudhuria kongamano hilo wamesema kupitia kongamano hilo wamepata elimu ya kuwa na mikataba pia kukumbuka kuweka akiba kwani matatizo hayapigi hodi.

“Tunashukuru sana kwa kongamano hili na tunaamini kuna mengi tumejifunza na tutayatumia na mafundi wengine tumekuwa sio waaminifu lakini kupitia hii itatusaidia kuwa waaminifu kwa sababu mambo mengi tunafanya kienyeji kama tulivyorithishwa na waze wetu"

Kongamano la Fundi Smart limehusisha zaidi ya mafundi 1800 ambao wampatiwa limu kupitia wadau mbalimbali huku kongamono hilo likienda katika ukanda mwingine .

MWISHO .


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: