Mtendaji wa Kampuni ya Solutions Tag Bw.Peter Kichogo (kulia) akisaini mkataba wa Kazi ya Kusafisha na Kukagua Bomba la Gesi Asilia.Mkataba huo wamesaini na kampuni ya Maurel and Prom Exploration Production Tanzania Ltd, Hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Machi 6, 2023. Meneja Mkuu kampuni ya Maurel and Prom Exploration Production Tanzania Ltd Bw.Nicolas Engel (kushoto) akisaini Mkataba wa Kazi ya Kusafisha na Kukagua Bomba la Gesi Asilia.Mkataba huo wamesaini na Solutions Tag Consulting Company Ltd ,Hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Machi 6, 2023.Meneja Mkuu kampuni ya Maurel and Prom Exploration Production Tanzania Ltd Bw.Nicolas Engel akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Solutions Tag Bw.Peter Kichogo wakionesha mkataba waliosaini wa Kazi ya Kusafisha na Kukagua Bomba la Gesi Asilia . Hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam Machi 6, 2023. Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau (LCSEU ) kutoka PURA, Charles Nyangi Kangoye akizungumza katika hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Kazi ya Kusafisha na Kukagua Bomba la Gesi Asilia Kati ya Maurel and Prom Exploration Production Tanzania Ltd na Solutions Tag Consulting Company Ltd Katika Hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo Machi 6, 2023.

**************************

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) leo Jumatatu Machi 06 ,2023 imeshuhudia hafla ya utiaji saini wa mkataba wa kazi ya kusafisha na kukagua bomba la gesi asilia kati ya kampuni ya Maurel and Prom Exploration Production Tanzania Ltd na Solutions Tag Consulting Company Ltd .

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Meneja Mkuu kampuni ya Maurel and Prom Exploration Production Tanzania Ltd Bw.Nicolas Engel amesema wao kama kampuni kupata kazi hiyo ni kutokana na kazi nzuri ambazo wameifanya katika miradi ya gesi na mafuta kwa zaidi ya miaka 10 na ni kielelezo cha kazi nzuri ambazo wamezifanya katika sekta hiyo ambayo inahitaji utaalamu wa hali ya juu .

Engel ameendelea kwa kusema kuwa, wao kufanya kazi na kampuni ya wazawa katika sekta ya gesi na mafuta ni katika mwendelezo wa azma yao ya kutaka kuacha alama katika eneo hilo.

"Tunataka kuacha alama nchini Tanzania kwa kushirikiana na kampuni za kitanzania hususan kampuni zinazojihusisha na miradi ya gesi na mafuta na gesi, na kwa kuanzia tumeanza na kampuni ya Solutions Tag Consulting Company Ltd"

Akizungumzia ushirikiano uliopo baina yao na PURA, meneja huyo amesema, mkataba uliosainiwa leo ni kielelezo cha ushirikiano mzuri kati yao na kuahidi kuendelea kufanya kazi hizo kwa ustadi mkubwa ili kudumisha matumizi endelevu ya bomba la gesi asilia.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau (LCSEU ) kutoka PURA, Charles Nyangi Kangoye ameeleza kuwa, miaka ya nyuma fursa ya wazawa na kampuni za Kitanzania kupata kazi katika mradi ya gesi na mafuta hazikuwepo lakini kutokana na jitihada za serikali kupitia PURA jambo hilo kwa sasa inawezekana.

"Miaka ya nyuma hizi fursa hazikuwepo, zimekuja sasa baada ya jitihada za serikali kwa kutengeneza sheria na kanuni ambazo PURA inazisimamia" Alisema Kangoye na kuongeza

"Tunawaomba Watanzania kuchangamkia fursa za mafuta na gesi zinapojitokeza, hivi karibuni tutaweka kwenye tovuti fursa zinazopatikana katika eneo la mafuta na gesi"

Kwa upande wake Peter Kichogo ,ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kitanzania ya Solutions Tag Consulting Company Ltd iliyopewa kazi ya kusafisha na kukagua bomba la gesi asilia amesema, hapo awali fursa hiyo waliyoipata wasingeweza kupata kwa kuwa kulikuwa hakuna wataalam wazawa wala kampuni za wazawa jambo ambalo lilipelekelea kampuni za nje kupata kazi hizo

"Sekta ya mafuta na gesi ni mojawapo ya sekta inayohitaji utaalamu wa hali ya juu, na kwa kuwa inahitaji utaalamu wa hali ya juu huduma za kitaalamu zilikuwa zinatoka nje, lakini sasa wazawa tunapata fursa hizi" alisema Kichogo.

Mkataba wa kazi ya kusafisha na kukagua (intelligent pigging)bomba la gesi asilia lenye urefu wa mita 800 linalotoa gesi asilia kutoka inapozalishwa katika kisima cha MB1 kilichopo cha Mnazi Bay (Mtwara) hadi uliopo mtambo wa kuchakata gesi wa Mnazi Bay unaoendeshwa na kampuni ya Maurel and Prom Exploration Production Tanzania Ltd.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: