Nahodha wa timu ya Kamba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Robert Keboya akipokea kombe la mahindi wa Kamba kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kicherebaada ya kukamilika kwa Bonanza la watumishi lililoamdaliwa na Ofisi ya CAGna kufanyika viwanja vya Kilimani Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Club ya Michezo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC SPORTS CLUB) Juvenile Kaiza akiwa na kombe hilo.Bingwa wa Netbal timu ya Ukaguzi ikikabidhiwa Kombe lake.
Bingwa wa Mpira wa Miguu, timu ya Makao Makuu Jogging Club wakikabidhiwa kombe lao.
Bingwa wa Mpira wa Miguu, timu ya Makao Makuu Jogging Club wakikabidhiwa kombe lao.
Mazoezi ya viungo na kukimbia Jogging vilifanyika kabla ya kuanza bonanza hilo.
Watumishi waliokuja na watoto wao wakipiga picha na CAG, Charles Kichere.
TIMU ya Kamba ya Tume ya Aifa ya Uchaguzi (NEC) imefanikiwa kutwaa kombe katika Bonanza la Ukaguzi lililofanyika Jijini Dodoma na kushirikisha timu zaidi ya sita.
Watumishi waliokuja na watoto wao wakipiga picha na CAG, Charles Kichere.
Wafukuza upepo nao walikuwepo
Mbio za magunia
Kukimbia na yao kwenye kijiko
Kufukuza kuku mahindi alikua timu ya NEC.
Timu Kamba ya NEC ikiwavuta Ukaguzi.
Mchezo wa Netbal nao ulikuwepo na Ukaguzi kutwaa ubingwa. TIMU ya Kamba ya Tume ya Aifa ya Uchaguzi (NEC) imefanikiwa kutwaa kombe katika Bonanza la Ukaguzi lililofanyika Jijini Dodoma na kushirikisha timu zaidi ya sita.
NEC ilitwaa ushindi huo baada ya kuwavu ta kwa mivuto miwili Timu ya Ukaguzi.
Katika Mpira wa Miguu NEC hawakufurukuta mbele ya Makao Makuu Jogging baada ya kuwatupa nje kwa mikwaju ya penati ambao badae katika fainali walikutana Ugakuzi na Makao Makuu na Makao Makuu kutwaa ubingwa wa Soka.
Katika mchezo wa Mpira wa Netball timu ya Ukaguzi iliibuka kidedea baada ya kuwatndika bila huruma timu za Wizara ya Afya na Madini.
Mapema akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ametoa rai kwa watumishi wa umma wakiwemo wa Ofisi yake kushiri kwenye michezo kwani ni tiba isiyo na gharama.
Taasisi zilizoshiriki mbali na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mfuko wa Bima ya Afya ya Uchaguzi(NHIF), Wakala wa Barabara(Tanroads) Ofisi ya Rais Ikulu na Wizara ya Afya.
Alisema ili kuwa na afya njema ni vyema watumishi wakashiriki mazoezi na kusisitiza kuwa mazoezi ni tiba isiyo na gharama kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na pia kuipunguzia Serikali mzigo wa kuhudumia magonjwa hayo.
"Kazi zetu sisi Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali tunatumia muda mwingi kuandika taarifa hivyo tumekuwa tukiweka utaratibu wa kutoka nje kufanya mazoezi na ni utaratibu mzuri katika kulinda afya za watumishi."
Kichere pia alisema wanatumia bonanza hilo kujiandaa tayari na bonazan lingine litakalokutanisha na wabunge.
" Wabunge ni watu ambao tunafanya kazi nao kwa karibu, hivyo mwezi ujao tutakuwa na bonanza la kushirikiana na wabunge kwa hiyo hii ni sehemu ya mazoezi yetu."
Kichere alisema katika bonanza Hilo pia watalitumia kuchagia damu benki ya Taifa ya damu Ili kusaidia kutoka maisha ya watu wanaohitaji damu.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya CAG, Novat Mfalamagoha kutokana na mtindo wa maisha ya mwanadamu mazoezi ni mabadala mzuri wa dawa za hospitali.
Pia alishauri wazazi kujenga tabia ya kuwashirikisha watoto kwenye mazoezi ambayo itawafanya kujenga moyo wa kupenda mazoezi.
Post A Comment: