Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinani Mpyagila amesisitiza wanaokopa mikopo ya asilimia 10 lazima warudishe kwa wakati la sio jela inawahusu( PICHA KUTOKA MAKTABA)


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinani Mpyagila ametangaza vita na vikundi vyote ambavyo vimekuwa havirudishi mikopo ya asilimia 10 wanayokopeshwa na Halmashauri hiyo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya LAAC, Mwenyekiti huyo alisema kuwa kumekuwa na vikundi vingi vinakopa lakini vinashindwa kurudisha fedha hizo kwa wakati au mara nyingine wasirudishe kabisa fedha hizo hivyo kamati ya LAAC imewapa nguvu ya kuwakamata wote ambao hawajarudisha fedha hizo na kuwapeleka mahakamani.

Mpyagila alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea itaendelea kutoa kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vyote kama ambavyo serikali imeagiza lakini watakuwa makini na wakali kwa wanavikundi wote wadanganyifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Injinia Chionda Kawawa alisema kuwa watakuwa makini mno wakati wa kutoa mikopo ya asilimia 10 ili kuepukana na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata kutoka kwa wananchi waliokopa kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Injinia Kawawa alisema kuwa kamati ya LAAC imewapa nguvu na njia muhimu za kufuatilia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kila kikundi kinarejesha mkopo kwa wakati na vikundi vingine viendelee kukopa.

Naye mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka wafanyakazi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuacha mara moja kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na Kasi ya serikali ya awamu ya sita.


Moyo alisema kuwa hatakuwa tayari kumvumilia mtendaji yoyote yule atakaye fanya kazi kwa mazoea katika wilaya ya Nachingwea.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: