Na Mwandishi wetu

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI imepatiwa Vifaa Tiba venye thamani ya Shilingi Bilioni 2 na Chuo Kikuu cha Weil Cornel cha New York Marekani.

Akizungumza wakati wa kuhihitimisha Kongamano la tisa la Kimataifa la mafunzo ya nadharia na  vitendo kuhusu upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu yaliyofanyika kwa siku tano jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt.Asha  Abdullah amesema kongamano hili la tisa limehudhuriwa na zaidi ya madaktari 200 kutoka nchi mbalimbali duniani ambapo mafunzo yametolewa na madaktari bingwa wa MOI na wengine kutoka Marekani.

“Mafunzo ya mwaka huu yamekuwa ya kipekee zaidi kwani wataalamu  kutoka chuo cha Weil Cornell wametuletea vifaa mbalimbali vinavyogharimu billioni 2 vilevile MOI yajenga historia kuwa wakwanza kumiliki vifaa vya aina hiyo Afrika Mashariki amesema Dkt Asha.

Akizungumza Mara baada ya kufanyika kwa operesheni hizo daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, uti wa mgongo a mishipa ya fahamu Dkt Hamisi Shabani amesema mafanikio ya upasuaji huo ni matokeo ya jitihada za serikali ya awamu ya sita kuupa kipaumbele sekta ya afya kwa kufanya uwekezaji mkubwa wa madaktari bingwa na vifaa tiba.

Kwaupande wake Dkt Laurent Mchome ambae pia ni mbobezi wa upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu amesema upasuaji uliofanyika leo Sio mara ya kwanza isipokuwa utaalamu katika upasuaji hubadilika mara kwa mara ndio maana tunashirikiana na wataalamu kutoka Weil Cornell ili kuongeza ufanisi katika suala zima la upasuaji nchini.

“Tulianza kwa kujifunza darasani ili tuangalie namna ya kushirikiana katika ujuzi na tukahamia kwenye nadharia ya vitendo lakini mikutano ya namna hii ni muhimu kwa sababu inakutanisha madaktari pamoja ameeleza Dkt Mchome

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wa chuo kikuu cha Weil Cornell Profesa Roger Hartl amesema ni heshima kubwa kufika Tanzania kwa mara nyingine ikiwa ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano. 

“Tunataka wenzetu wa MOI na madaktari waliopo mafunzoni waweze kutoa huduma hizo kwa weledi mkubwa na tumekuwa tukifanya hivi kwa zaidi ya miaka 10 na hivyo kupelekea programu hii kujulikana kimataifa amesema Profesa Roger Hartl.

Ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Marekani ni kielelezo kizuri cha kuwepo kwa mafunzo hayo.



Share To:

Post A Comment: