*******************
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukioongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt Angeline Mabula.
Viongozi hao wamekutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 13 Machi 2023 katika ofisi za wizara zilizopo katika mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.
Viongozi aliokutana nao Mkurugenzi Mkuu wa NHC ni pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Anthony Sanga.
Bw. Hamad Abdallah ameteuliwa hivi karibuni kuwa mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kuchukua nafasi ya Nehemiah Mchechu aliyeteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.
Post A Comment: