Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo alipozungumza na wakazi na wanachama wa CCM Shina namba 5, Tawi la Iguguno Kaskazini, Kata ya Iguguno wilaya ya Mkalama.
Na Dotto Mwaibale, Mkalama
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida James Mkwega
amemuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Daniel Chongolo kuongeza idadi ya walimu ambao hawatoshi wilayani
humo.
Mkwega alitoa ombi hilo kwa Chongolo wakati wa siku ya nne ya ziara yake ya
kukagua ilani ya chama hicho na kukagua miradi ya maendeleo wakati akizungumza
na wananchi wa shina namba tano Kata ya Iguguno Machi 2, 2023.
"Ndugu Katibu Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya
kutoa fedha na kujenga madarasa katika halmashauri yetu lakini changamoto kubwa
iliyopo hatuna walimu wa kutosha tunaomba ukatuombee hatusaidie katika
hilo" alisema Mkwega.
Chongolo akielezea changamoto hiyo alimuhakikishia Mkwega kuwa jambo hilo
atalifanyia kazi na kuangalia usawa wa walimu waliopo kati ya mjini na
vijijini.
Wakati huohuo Chongolo amesema atakwenda kuwaona wahusika na kuwahakikishia
wananchi wa wilaya hiyo kujengwa kwa barabara ya kiwango cha lami kutoka
Iguguno hadiimakao makuu ya wilaya ya Mkalama Nduguti.
Aidha Chongolo alisema barabara hiyo haitaishia Nduguti pekee bali itafika
hadi Sibiti wilayani humo, Meatu mkoani Shinyanga na kuunganisha mikoa ya
Manyara na Arusha.
Chongolo alitoa maelezo hayo kufuatia ombi lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki Francis Isack kuomba kujengwa kwa barabara hiyo ya kilometa 42.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Sophia Mjema akizungumza kwenye mkutano huo. |
Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Singida,Martha Mlata akizungumza kwenye mkutano huo.
Post A Comment: