Na;Elizabeth Paulo, Dodoma
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ipo Katika Mageuzi Makubwa ya Sekta ya Elimu Ambapo Mageuzi Hayo Yanaanzia Ngazi Ya Chini Mpaka Kufikia ngazi za juu.
NAIBU KATIBU Mkuu Wizara Ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, Ameyasema Hayo Leo Machi 16,2023 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza wakati wa Kongamano la kujadili namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB).
Amesema lengo la Mkutano huo ni kuangalia mbinu na njia bora ambazo zitasaidia kupata fedha zitakazo Kuwa endelevu kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo kusoma na kufanya majadiliano ya kujua namna elimu ya leo inavyotolewa kama inatoa ujuzi kwa vijana kujiajiri.
"Cha msingi ni kujadili mbinu bora ambazo zitakuja kusaidia kupata vyanzo mbadala vya kusomesha vijana wetu ambao Serikali inakwenda kufanya mageuzi makubwa ya Elimu.
"Tutakuwa na wanafunzi wengi wanaosoma kulingana na soko la ajira, lazima watoke na ujuzi ambao watapata ajira huko mitaani baada ya kusoma".Alisema Rwezimula
Naibu katibu huyo amesema kwa hivi Sasa wameshapata wadau ambao ni Benki Ya NMB na tayari wameshaanzisha programu inayoitwa "ELIMU LOAN" ambapo wametenga Bilioni 200 ambazo watu wataenda kukopa hususani wafanyakazi wa Serikali na Sekta Binafsi kwa riba ndogo ya asilimia 9%.
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Bodi Ya Mikopo Tanzania Bara Professa. Khamis Ndihega Amesema mwaka huu 2023 wanafunzi zaidi ya elfu 70,000 ambao wanaingia vyuoni na kuweza Kupata mikopo na kusema idadi hiyo ni kubwa na imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
"Kila mmoja ambaye yupo na uwezo anastahili apate nikopo, kama mnavyojua kinachotazamwa kwenye Bodi za Mikopo ni ule uwezo wa wazazi kuhakikisha kwamba wanaweza kumpeleka mtoto wao Chuo Kikuu sasa hii Sio wengi wanao Uwezo huo".Alisema Prof. Ndihenga
Nae Mwenyekiti Wa Bodi Ya Mikopo Zanzibar, Ndg.Mohammed Hafidh Khalfan Amesema mkutano huo ni katika kutafakari yale yanayojitokeza juu ya mikopo, Tulipotoka, Tulipo na Vipi Tunajiandaa Tunapokwenda Ili hatimae Vijana( Ambao ni Wanafunzi)waweze Kupata Fursa Ya Mikopo.
Post A Comment: