Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita ndani ya kipindi cha miaka miwili tangu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan aingie madarakani katika mkutano uliofanyika jana Machi 18, 2023 Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


Na Dotto Mwaibale, Singida

ILI kuunga mkono mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii yaliyofikiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake, viongozi wa dini mkoani hapa, wamewataka wakuu wa idara zote serikalini kuweka mbele uadilifu na uaminifu katika matumizi ya fedha wana po tekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Wametoa nasaha hizo jana Machi 18, 2023 wakati wa mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoahuu, Peter Serukamba kubainisha mafanikio ya miaka Miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tumesikia hapa fedha zilizotolewa na Rais kwa ajili ya miradi mbalimbali yamaendeleo kwa mkoa wetu (Singida), nitoe mwito kwa idara zote wawe waadilifu katika matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Ni vizurizitumike kulingana na taratibu, viongozi wawe waadilifu, wazipokee na kuzitumia katika unyenyekevu, waige mfano wa Rais (Mama Samia) mwenyewe mnyenyekevu na mpole wawe na huruma na upendo na watu.

“Viongozi msiishie kusema mama anaupiga mwingi, taarifa ya leo ni hatua nzuri kwa taifa letu,” alisema Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kati, Dk. SyprianHilinti, amewataka watendaji wanaomsaidia Rais mkoani hapa watekeleze miradi ya maendeleo kwa haraka, ubora na mafanikio.

Alimpongeza Rais Samia kwa uongozi wenye kasi yenye upendo na hekima na kwamba anamwombea aongoze kwa uadilifu na amani.

Aidha, alimshukuru mkuu wa mkoa Serukamba kwa kuwa kiongozi wa mfano mkoani hapa katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kimaendeleo.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Edward Mapunda,alisema maendeleo makubwa aliyoyafanya Rais Samia katika kipindi cha miaka miwili ni ya Watanzania wote,hivyo ni vema wamwombee kwa Mungu aliyetaka wakati huu awe rais wa Taifa hili ili azidi kutekeleza majukumu aliyoitiwa na Mungu.

Awali Serukamba alisema katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa  Rais Samia miradi mingi ya kijamii na kiuchumi imetekelezwa mkoani hapa kutokana na bajeti ya  mkoa kuongezwa zaidi ya mara dufu.

“Bajeti ya sekretarieti ya mkoa imeongezeka kutoka sh. Milioni 180,187,060,500 mwaka 2020/2021 hadishilingi 239,808,971,000 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 33.09,” alisemaSerukamba.

Aidha, alibainisha kuwa Serikali Kuu imeidhinisha bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa mwaka 2022/2023 kwa ajili ya kuwalipa posho madiwani na watendaji kata na posho za mawasiliano kwa watendaji wa vijiji kitendo ambacho hakikuwahi kufanyika katika awamu zote za serikali zilizopita.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro Issa akizungumzakatika mkutano huo kabla ya kumuombea dua Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwaambayo nchi imeyapata katika kipindi cha miaka miwili tangu aingie madarakani.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati  Dkt. Sprian Hilint akizungumza katika mkutano huo.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Edward Mapunda (katikati) akiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Taswira ya mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu (wa pili kulia) akiwa kwenye mkutano huo.
 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: