Na Denis Chambi, Tanga.
Matokeo
chanya ya maboresho yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika bandari ya Tanga yanaendelea
kuonekana kufwatia meli kubwa za mizigo kutoka nje ya nchi zikiendelea
kutia nanga wafanyabiashara wakizidi kuitumia hatua ambayo inakwenda
kuongeza biashara shindani katika ukanda wa Afrika mashariki.
Ukiachana
na meli kubwa iliyopokelewa hivi karibuni imeendelea kuwa mwendelezo
ambapo bandari hiyo imepokea nyingine yenye urefu wa mita 150 kutoka
china iliyobeba Clinka ya kiwanda cha Lime stone kilichopo mkoani hapa
huku wakitarajia kupokea meli nyingine yenye urefu wa mita 189.9 hii
ikionyesha mapinduzi ya kibiashara ambayo yatazidi kuifungua Tanga.
Bandari
ya Tanga imeanza kuhudumia meli kubwa ya mizigo yenye urefu wa mita 179
meli ambayo imekuja na magari ikiwa ni mara ya kwanza kushushwa magari
bandarini hapo baada ya maboresho ya ujenzi wa gati lenye urefu wa mita
450.
Meli hiyo iliyotokea
Nchini China ni meli ya kwanza kuja na magari katika bandari ya Tanga
tofauti na meli nyingine ambazo zilishakwisha kutia nanga bandarini hapo
mara baada ya kukamilika kwa maboresho hayo.
Ukiachana
na meli kubwa yenye urefu wa mita 150 iliyopokelewa hivi karibuni
katika bandari ya Tanga imeendelea kuwa mwendelezo ambapo bandari hiyo
kwa mara nyingine imepokea meli yenye urefu wa mita 179 kutoka Nchini
China iliyobeba magari na vifaa vya kiwanda cha Maweni Lime stone
kilichopo Mkoani hapa huku wakitarajia kupokea meli nyingine yenye urefu
wa mita 189.9 hii ikionyesha mapinduzi ya kibiashara ambayo yatazidi
kuifungua Tanga'.
Akizungumza
wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa bandari
hiyo mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba aliyekuja na kauli mbiu ya
'Tanga lango kuu la Afrika Mashariki amesema kuwa wanaitazama bandari ya
Tanga kimkakati zaidi na kuwaasa wafanyabiashara mbalimbali wa kutoka
ndani ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kuitumia bandari ya
Tanga ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwao katika kusafirisha mizigo
yao kwa haraka zaidi.
"Niwaombe
wafanyabiashara wote wa ndani na nje ya Tanga kutumia bandari yetu ya
Tanga lakini pia niwasisitize majirani zetu wa Rwanda, Burundi,
Congo, Kenya na kwingineko waangalie bandari ya Tanga kama changuo lao
namba moja, "alibainisha Kindamba.
"Bandari
hii ndio moyo wa uchumi wa Mkoa wa Tanga sisi kama wasimamizi wa
serikali tunakwenda kuisimamia bandari hii kwa ukaribu zaidi tunataka
Dunia ijue kwamba ipo bandari inayoitwa bandari ya Tanga tena ikiwa na
usalama mkubwa kabisa, "alisisitiza Kindamba.
Aidha
amewaomba wafanyabiashara mbalkmbali wa kutoka ndani ya Tanzania na
nchi za Afrika Mashariki kuzidi kuitumia bandari hiyo ambayo itakuwa na
manufaa kwao huku akiwataka wa wafanyakazi wa bandari hiyo kuendelea
kudumisha mahusiano baina yao.
"Kuwaomba
wafanyabiashara wote wa ndani na nje ya Tanga kutumia bandari ya Tanga ,
kuwaomba majirani zetu Rwanda , Burundi Congo Kenya na kwingineko
waangalie bandari ya Tanga kama changuo lao namba moja na sisi
tunakwenda kuisimamia bandari hii kwa ukaribu zaidi na ndani ya kupindi
kifupi watu watakaa na kuizungumzia bandari ya Tanga ambayo haijawahi
kuzungumzwa tena tutakuwa tunavunja rekodi zetu sisi wenyewe kwa
wenyewe, tunataka dunia ijue kwamba ipo bandari inaitwa Tanga" alisema
Kindamba.
Meneja
wa bandari ya Tanga Masoud Mrisha pamoja na maboresho hayo
yaliyofanyika ameiomba serikali kupitia wakala wa barabara za mijini na
vijijini TARURA na TANROADS kutengenezwa kwa miundombinu ya barabara ya
kilomita 7 inayokwwnda Mwambani kwenye bandari ndogo ambako wanatarajia
kujenga
"Wote
tunafahamu kwamba bandari ndio moyo wa biashara kwa mkoa wa Tanga
mkuuwa mkoa tulimwomba atusaidie ndungu zetu wa Tanroads na TARURA
kututebgenezea ile barabara kutoka hapa mpaka mwambani kilomita 7 kule
tunatarajia kujenga sehemu ya kuhifadhia mizigo yetu sote tunafahamu
bandari yetu ya Tanva ina ukubwa wa hekta 17 eneo hili sio kubwa sana
tumemwomba mkuu wa mkoa atusaidie kututilia nguvu kwenye hizo taasisi"
alisema Mrisha.
"Niiombe
Serikali kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura na
Tanroads kutengenezwa kwa miundombinu ya barabara ya kilomita 7
inayokwenda Mwambani kwenye bandari ndogo kule tunatarajia kujenga
sehemu ya kuhifadhia mizigo yetu sote tunafahamu bandari yetu ya Tanga
ina ukubwa wa hekta 17 eneo hili sio kubwa sana tumemwomba mkuu wa mkoa
atusaidie kututilia nguvu kwenye hizo taasisi" alisema Mrisha
Serikali
imewekeza kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 429 kwenye bandari ya
Tanga kwajili ya ujenzi wa gati, kuongeza kina cha maji na ununuzi wa
mitambo kwajili ya kuwezesha bandari hiyo kuhudumia meli kubwa ambazo
zilikuwa zinashindwa kutia nanga bandarini hapo.
Hata hivyo serikali inatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa mradi wa gati katika bandaro hiyo ifikapo mwezi April mwaka huu.
Meli yenye ukubwa wa urefu wa mita 179 ambayo imekuja na mzigo magari na Clinca kutoka China ikiwa ni mara ya kwanza kutia nanga
bandarini hapo baada ya maboresho ya ujenzi wa gati mbili zenye urefu wa mita
450.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya ziara yake ya kutembelea bandari ya Tanga na kuzungumza na wafanyakazi march 15, 2023. kushoto kwake ni meneja wa bandari hiyo Masoud Mrisha.
.
Post A Comment: