Denis Chambi, Tanga.
MTEGO
uliowekwa na jeshi la uhamiaji mkoa wa Tanga umefanikiwa kuwanasa
Mawakala wanne waliokuwa wanajihusisha na biashara haramu ya usafirshaji
wa binadam waliokuwa wamewahifadhi katika nyumba ya mmoja wao iliyoko
Muheza mkoani Tanga .
Akizungumza
na waandiahi wa habari ofisini kwake kamanda wa uhamiaji mkoa wa
Tanga Kagimbo Bakari amesema kuwa kwa kipindi cha muda wamekuwa
wakipambana kuweka mbinu mbalimbali z kuweza kuwabaini wale wote
wanaojihusisha na biashara hiyo ambapo wamefanikiwa kuwakaata na tayari
wamefikishwa mahakamani.
Amewataja
mawakala hao kuwa ni Joseph Thimothi mwewnye nyumba walimokuwa
wamehifadhiwa wahamiaji hao, wengine ni Charles Mwapela Kimaki
Maneno, Athuman Mwameja pamoja Majoka Kipala wote hawa wakiwa ni raia
wa Tanzania.
"Hawa ni
mawakala ambao wanahusika na usafirishaji haramu wa binadamu karibu
nyakati zote tumekuwa tukipambana kutafuta mawakala na tumewapata
kutokana na mahusiano ya kesi ambazo nyingine ziko zinaendelea
mahakamani na watuhumiwa wote tumewafikisha katika ofisi ya uhamiaji
mkoa wa Tanga na mahojiano bado yanaendelea" alisema Kamanda Bakari
Aidha
katika taarifa nyingine Jeshi la uhamiaji mkoa wa Tanga march 10, 2023
limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haram wanne raia wa Cameroon katika
nyumba za kulala wageni jijini hapa wakidai kuwa wamekuja kwaajili ya
kufanya mazoezi ya kujiunga na timu za Coastal Union na African Sports
ambapo wameletwa na wakala wao aliyefahamika kwa jina la Benard
Matomondo Mfaume.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa uhamiaji mkoa wa Tanga
Kagimbo Bakari alieleza kuwa raia hao ambao waliingia hapa nchini
kupitia uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) na hatimaye
kufanikiwa kupata visa ya matembezi (HV) za siku 90 badala ya visa za
kibiashara (BV) kulingana na shughuli walizokuja kuzifanya.
"March10,
2023 usiku katika nyumba ya kulala wageni ya New MayLodge na New Palm
Life zilizopo jiji la Tanga barabara ya 4 na 20 walikamatwa raia
wanne wa Cameroon walikuja mkoa wa wanavyodai wao wamekuja katika timu
za Coastal Union na African Sports kufanya mazoezi ili kujiunga na timu
hizo kwa msaada wa wakala wao wa michezo aitwaye Benard Mtomondo
Mfaume anaishi Dar es salaam"
"Uchunguzi
wa awali unaonyesha raia hawa wa Cameroon waliingia kupitia uwanja wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JKNIA na kupata viza za
matembezi ya siku 90 na sio za kufanya shughuli zozote za michezo na
wapo hapa tayari kwa kufanya mazoezi ili waweze kisajiliwa katika timu
hizo za Coastal Union na African Sports" alisema Kamanda Bakari.
Hata
hiyo kamanda huyo alibainisha kuwa mara baada ya kuwakamata raia hao
waliwaita viongozi wa timu za African Sports na Coastal ambao
walikanusha kutokuwatambua wala kuwa na mawasiliano nao na barua
walizokuwa nazo zote ni za kughushi na paspoti walizokuwa nazo sio
sahihi.
"Uchunguzi
uliofanyika katika timu ya Coastal Union kupitia kwa katibu wa klabu
anaeleza kutokuwatambua wala kuwafahamu na wala hana mawasiliano nao
kwa mfano barua zote walizonazo ni za kughushi sii barua sahihi na
paspoti walizo nazo sio paspoti sahihi kwa mujibu wa viongozi wa Coastal
Union kwamba hawajawahi kuwaona wala hawahusiki nao"
"Kwa
upande wa African Sports wao wameeleza kutokuwatambua na kwamba wana
barua ya Fountain Get na Pamba Football klabu bado wakala wao wa michezo
tunaendelea kumtafuta kwani hapokei simu ili tuweze kujua anaye
wahudumia hapa mkoani Tang alielezaKamanda huyo.
Aliwataja
majina raia hao kuwa ni Romanus Gwa, Cedric Donald Pouanguae Tchchoua,
Sainsburunde Nji, pamoja na RowandBenard Messi Tangana.
Post A Comment: